………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MBUNGE Viti Maalum ,mkoa wa Pwani Alice Kaijage ameeleza kuwa ,Taifa linapaswa kuendelea kuilinda amani na utulivu ili kuwaenzi waasisi wetu waliopigania uhuru.
Pamoja na Hilo ,ameliomba Taifa liendelee kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza nchi kwa amani ili kutimiza adhma ya kuinua uchumi wa nchi.
Alice aliyaeleza hayo wakati wanawake wa UWT Kibaha Mjini walipounga mkono Taifa kusheherekea siku ya Uhuru pamoja na hilo kumpongeza Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja kutimiza miaka 60 .
Alice alifafanua ,wananchi tuendelee kutembea kifua mbele kwa amani iliyopo ,Ni tunu ya Taifa Kwani Taifa limekuwa mfano kwa mataifa mengine kwa kuilinda amani na kuwa na utulivu.
Aidha aliwaasa wanawake kujituma kwa kushirikiana na familia ili kujikomboa kifamilia na kiuchumi.
“Kilio Cha Rais Samia Ni kuona mwanamke anajikomboa kiuchumi ,na kufanya kazi kwa bidiii ili kurahisisha mambo ,Kwani kina mama wanafanya kazi kubwa kuhakikisha Rais anasimama imara na kufanya kazi kwa utulivu “alifafanua Alice.
Vilevile , anasema Serikali imeendelea kufanya makubwa kwa mshikamano kupitia viongozi waliopita kwa hatua.
Kuhusu baadhi ya vituo vya afya Kibaha Mjini kulalamikiwa kufungwa mapema na kushindwa kufunguliwa kwa wakati ,Alice alisema amelibeba tatizo hilo na atakwenda kulifanyia kazi.
Awali mama Elina Mgonja alimshukuru mungu kutimiza miaka 60 na kuunganisha shughuli hiyo na sherehe za uhuru .
“So rahisi ,Ila kwa kudra za mungu nimefika ,Rai yangu wanawake tushirikiane ,tuachane na majungu na kukatishana tamaa ,Mambo hayo yamepitwa na wakati ,Tuwe na umoja kupiga hatua kimaendeleo”alisema Mgonja.
Mgonja alieleza ,UWT ya Sasa imepiga hatua na wanaendelea kutoa elimu za ujasiliamali ,na hatua hiyo imetokana na viongozi mbalimbali walioshika nafasi za kuongoza wilaya na wanawake wenyewe.
Aliipongeza Serikali kuboresha sekta ya afya na maji Kibaha Mjini kuhakikisha inatatua changamoto hizo kwa wanawake waliopata tabu miaka iliyopita kuzaa chini ,mlundikano katika vituo vya afya ,vifo vya watoto chini ya miaka mitano na kuboresha wodi za uzazi na upasuaji.
Mgonja alibainisha wanaendelea kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanawake na ujenzi wa jengo la duka maalum la kuuzia bidhaa zao ili kumkomboa mwanamke.
Mjasiriamali Rehema Selemani mkazi wa Pangani Kibaha , alieleza kwamba amepata elimu ya ujasiliamali kupitia UWT Kibaha na Sasa anaweza kunufaika kwa kutengeneza batiki na sabuni.
Kutokana na jitihada za UWT Kibaha Mjini,mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, alifurahishwa na jitihada za wanawake wajasiliamali ambapo pia wameanzisha bidhaa ya mafuta na sabuni yanayotengenezwa kwa kutumia majani ya ufuta ,Mwani na mlenda .
Kunenge aliielekeza Halmashauri ya Mji wa Kibaha kuwatupia macho na kuwashauri,watangaze bidhaa hiyo iweze kuwa yenye viwango na ubora ili ipate soko kirahisi ndani na kimataifa.