KAMISHNA wa Bajeti Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Bi. Saumu Khatib Haji (mwenye miwani) akiwafanyika uhakiki baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja walioekeza fedha zao katika Kampuni ya Masterlife, iliyokuwa ikifanyakazi kinyume cha Sheria, ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, aliahidi kurejeshewa fedha zao. Zoezi hilo kwa awamu ya kwanza limeaza katika Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkotoni leo 8-12-202, litakuwa kwa siku tatu hadi 10-12-2021.(Picha na Ikulu)
MAOFISA kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar. wakiendelea na zoezi la kumfanyia uhakiki Mwananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae aliweka fedha zake katika Kampuni ya Masterlife, iliyokuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, aliahidi kurejeshewa Wananchi fedha zao, zoezi hilo kwa awamu ya kwanza limeaza leo 8-12-2021 na kumalizika 10-12-202, katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
MWANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja akihesabu fedha zake baada ya kukabidhiwa na Maofisa wa kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.Ndg.Sabri Udi (mwenye fulana nyeusi) na kushoto kwake) Ndg. Issa Salum , zoezi hilo la kuwarejeshea Fedha zao Wananchi hao waliowekeza katika Kampuni ya Masterlife kwa awamu ya Kwanza wameaza kulipwa walioweleza shilingi laki moja hadi milioni moja, limeaza leo kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, 8-12-2021 hadi 10-12-2021.(Picha na Ikulu)
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akisimamia zoezi la kurejeshewa Fedha Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,waliowekeza katika Kampuni ya Masterlife iliyokuwa ikifanyakazi kinyume cha sheria, zoezi hilo lililofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni Unguja leo 8-12-202 hadi 10-12-2021 kwa awamu ya kwanza kwa Wananchi walioekeza kuazia shilingi laki moja hadi milioni moja.(Picha na Ikulu)