Diwani wa Kata ya Mikocheni Eng Nzenzely Hussein katikaki wakiwa kwenye ukaguzi wa miradi ndani ya Kata ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama. Mradi wa vyumba vya madarasa ya Ghorofa na Maabara tatu (3) Kemia, Fizikia na Baiolojia shule ya sekondari Mikocheni.
Barabara ya regent iliyo kamilika kwa kiwango cha lami.
Barabara ya Chwaku ikiwa katika matengenezo.
Mradi wa kisima cha maji uliopo mikocheni mtaa wa darajani kilichofaziliwa na YilmazMehmet Ali Dertop.
*****************
Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mikocheni kikiongozwa na Diwani wa kata hiyo Mhandisi Nzenzely Iddy akiambata na watendaji wa kata, mitaa na viongozi wa kamati ya (CCM ) wametembelea miradi inayotekelezwa na ilani ya Chama.
Katika ziara hiyo wametembelea mradi wa kisima cha maji uliopo Mikocheni A ambao unajumuisha jumla ya visima 16 vilivyo jengwa katika kata hiyo ambavyo vimepunguza hadha ya upatikanaji wa maji ambao ulikuwa changamoto kwenye kata hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Angel Michele amesema ujenzi unaendelea vizuri mpaka kufikia mwezi wa kwanza mradi utakuwa umekamilika.
Nae Mkuu wa shule ya Sekondari Mikocheni A Bw.Hamisi Malela amesema kujengwa kwa maabara kutaongeza ufaulu kwasababu shule hiyo inafanya vizuri katika masomo ya sayansi wakiwa hawana maabara wanatumia madarasa.