**************
Na Imma Msumba, Ngorongoro
Mkuu wa wilaya Ngorongoro Mkoani Arusha Raymond Mangwala amefunga mafunzo ya jeshi la akiba ambapo mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika tarafa ya Ngorongoro.
Akifunga mafunzo hayo Mangwala amewapongeza wakufunzi wa mafunzo na wale wote walioshiriki mafunzo hayo na hatimaye kumaliza mafunzo hayo kwani ilikuwa ni safari ndefu mpaka kuhitimu mafunzo hayo
Mangwala amesema kuwa ana imani kuwa mafunzo hayo yamewajengea ukakamavu ujasiri na kujiamini kwani kwa sasa wahitimu watakuwa tofauti na wasiofanya mafunzo hayo
“Nina imani ndugu zangu mafunzo haya yatasaidia sana kwenye ukakamvu kwani mtakuwa ni tofauti kabisa na wasio fanya mafunzo ya mgambo kwani kwa sasa mtakuwa na hali ya kujiaminina kuwa wajasiri kutokana n mafunzo mliyopata”
Aidha ameongeza kuwa wahitimu hao wanatakiwa kujua ulinzi wa nchi ni wa wananchi wenyewe hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ulinzi wa nchi na kujilinda wao na familia zao.
Kwa upande wa mshauri wa mgambo wilayani Ngorongoro amesema kuwa mafunzo hayo yalianza yakiwa na jumla ya wanafunzi 81 na ilipungua hadi kufikia 51 waliohitimu kwani wengine walishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na utoro na magonjwa mbali mbali.
“Mheshiwa mgeni rasmi wanafunzi hawa walianza wakiwa 81 lakini kutokana na sababu mbalimbali wengine waliacha kutokana na sababu kama vile utoro,afya na kushindwa kumaliza mafunzo na hvyo kufanya wanaohitimu kuwa ni wanafunzi 51” Mshauri wa Mgambo