MKUU wa wilaya ya Tabora mjini Dkt Yahaya Nawanda
………………………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
MKUU wa wilaya ya Tabora mjini Dkt Yahaya Nawanda amewwataka watu wanaojihusisha na wizi wa miundombinu na alama za barabara waache kujiuhusisha na wizi huo kwani serikali itachukua hatua kali dhidi yao.
Hatua hiyo ya mkuu wa wilaya imekuja hasa baada ya alama za barabarani kwa baadhi ya maeneo kadhaa kung`olewa na kuibwa..
Akizungumza na gazeti hili ofisisni kwake Dkt Nawanda alisema wananchi wanapaswa kuwa na uchungu na uharibifu na wizi unaofanyika kwani serikali inatoa na kutu8mia fedha nyingi kutengeneza barabara hizo.
Alisema wananchi ni lazima wawe na uzalendo wa nchi na mali zao hivyo barabara hizi ni kodi zao kufanya hujuma na wizi ni jambo ambalo halitavumilika na atakayebainika atachukukuliwa hatua kali kwani atahesabika kama muhujumu uchumi uchumi.
Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kuwa barabara hizi ni mali za wananchi wenyewe hivyo jamii kwa ujumla inatakiwa kuwa na uzalendo na uchungu dhidi ya ugharibifu huo unaofanyika.
Dkt Nawanda aliwataka pia wale wote wanajihusisha na kufanya biashara ya ununuaji wa alama za baraarabni kuacha mara moja hujuma kwani serikali itapoawabaini haitasita kwachukulia hatua kali.
“Nawataka na kuwasihi wanaofanya biashara ya vyuma chakavu wasiingie kwenye mtego wa baadhi ya wanaoharibu alama za barabarani na kuwauzia serikali itawakamata na kuwapeleka mahamakani”alisema Dkt Nawanda.
Alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa polisi ama vyombo vya usalama pale wanapobaini wizi pamoja na watu wanajihusisha na hujuma hizo ili sheria ichukue mkondo wake.
Alisema kuwa watu wanaofanya wizi na uharibifu wa miuondombinu ya barabara wanaishi na jamii inayowazunguka kwa ujumla na wanafahamika hivyo muda sasa wananchi wanapaswa kuwataja na kuwafichua ili serikali iwashughulikie kwa ukalimifu.