***************************
Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuboresha sekta ya afya ameungana na wananchi wa kata ya mail moja kwa lengo la kuanza mradi wa ujenzi kwa ajili ya zahanati ili kuwaondolea adha ya kutembea umbari mrefu.
Akizungumza katika mkutano wa adhara kwa wananchi wa kata ya maili moja wakati wa ziara yake ya kikazi kwa lengo la kusikiliza changamoto za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.
Koka katika ziara hiyo ambayo ameambatana na viongozi mbali mbali wa serikali,wakuu wa idara pamoja na viongozi wa Chama ambapo wameweza kutembelea katika miradi ya sekta ya elimu elimu,miundombinu ya barabara,pamoja na kugagua ujenzi wa madarasa.
Aidha Koka alifafanua kwamba pamoja na kupambana ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambayo imejengwa katika eneo la Lulanza lakini pia atahakikisha anapeleka huduma ya afya katika maeneo yaliyopo pembezoni.
Kadhalika ametoa maelekezo kwa Tarura kuhakikisha wanazikarabati barabara kwa kuziweka kiwango cha changarawe ikiwemo na kuweka makaravati ili ziweze kupitika kwa urahisi hasa katika kipindi Cha mvua.
Nao baadhi ya wananchi kutoka mitaa ya msufini na muheza wamemuomba Mbunge kuwasaidia katika suala zima la ujenzi wa miundombinu ya barabara,maji,umeme pamoja na kuboesha huduma ya afya.
Pia amemchangia kiasi Cha shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaaa wa mail moja A ili kutoa fursa ya wananchi kupeleka changamoto zao.
Sambamba na hilo katika kuchagiza zaidi maendeleo atahakikisha anashirikiana bega kwa bega katika kuchangia miradi mbali mbali ya maendeleo na kwamba lengo lake ni kupunguza kero na changamoto zao.