……………………………………………………………
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
Rai hiyo ilitolewa jana na Sheikhe Msafiri Kitumbo, kutoka Shinyanga, kwenye maulidi na harambee ya kuchangia fedha za kukunua kiwanja kwa ajili ya upanuzi wa Msikiti wa Jihad, Nyabusalu Kata ya Kiseke, Manispaa ya Ilemela.
Alisema jamii na waumini wa Kiislamu wanapaswa kutambua umuhimu wa kuwathamini walimu na kuweke muda na gharama zao na kuwapatia vijana elimu ili kujenga taifa na kizazi chenye weledi wa kumcha na kumtumikia Mwenyezi Mungu.
“Madrasa zinaandaa vijana katika mabadiliko ya ujan ili wsinaswe na changamoto za kidunia,matatizo ya kimwili na mengine yanayotumbuka leo yanasababishwa na matumizi mbaya ya maisha ya ujana (anasa),pia madrasa zinatusaidia kuwajenga vijana kiroho na kuwa na hofu ya Mungu wanapopita kwenye changamoto za ujana,”alisema Sheikhe Kitumbo.
Alisema kuwa thamani ya walimu wakiwemo wa madrasa (walimu wa dini)imedogoswa hali inayoweza kusababisha taifa kuangamia,wanastahili kupewa thamani na hadhi yao kutokana na kutuandalia watoto wetu.
Sheikhe Kitumbo alisistiza walimu kukosa haki,kudharauliwa na kutothaminiwa ni kuliangamiza taifa wakati mbunge kazi isiyo ya kitaaluma anapata maslahi mazuri kushinda walimu.
“Uadilifu ni kumpa haki yake mtu usiyempenda kwa sababu unayempenda utampendelea tu,kiongozi ukiwa mwadilifu,wa kutenda haki huwezi kuwaogopa unaowaongoza hivyo lazima tuwape walimu thamani yao,”alisema
Sheikhe huyo alieleza kuwa yapo makosa watu wanaacha kuyatenda si kwa sababu ya kumuogopa Mungu bali kulinda heshima zao kwamba mtu anaweza asione mengi aliyo nayo,akikosa kimoja atasikitikana kutolea mfano kanuni ya 99 kuwa mtu mmoja alipewa bahasha yenye sh.99,000 ndani,juu ikiwa imeandikwa sh. 100,000,alipoikosa sh.1,000 hakulala usingizi akabaki kusikitika.
Kuhusu maulidi, Sheikhe Kitumbo alisema waislamu wanafahamu ni kusanyiko la kumuenzi Mtume Muhammad S.A.W.lakini kwa sasa roho ya ukarimu imetoweka na kusababisha watu kushindwa kutembeleana.
“Ugumu wa kutembeleana unachangiwa na roho mbaya si sababu ya hali mbaya ya kiuchumi wakati miundombinu bora tunayo,wazee wetu walitembelea kwa sababu walikuwa na roho nzuri,leo maulidi inatusaidia kula pamoja.Ukisikia msomaji wa Quran yeyote vuta tswira kuwa unaisikia sauti ya Mwenyezi Mungu,” alisema sheikhe huyo na kuwaasa waislamu kurejea kenye ukarimu.
Naye Sheikhe Mohamed Mbega,alisema wapo watu wanapingana kuhusu maulidi na vipo vitu utotoni vina athari kubwa ambavyo mtu akivikumbuka anajizuia kuvifanya.
“Maulidi tunaambizana mambo ya dini.Je, lini ningesimama Kiseke au Ilemela isingekuwa maulidi, ‘iwe jua, iwe mvua, tutakufa lakini lazima Mtume aswaliwe hapa’,mtu mwenye tabia nzuri hawezi kuwa mgeni wa maulidi na wanaotaka kuingia kwenye heri sharti watoe sadaka na zaka na waislamu hatuwezi kujiweka kando na sadaka pamoja na zaka,ni kukaribisha umasikini,”alisema.
“Mtu ana fail (anashindwa) sababu ya mipango dhaifu na hakuna akili bila kubuni mipango nah ii ndiyo tswira ninayoina Mwanza leo,nafasi za viongozi huko nyuma waligeuka kuwa waganga wa kienyeji na walijipamba kwa kazi kubwa ya kusubiri waumini msikitini,wakiwa nyumbani kusubiri wateja,sasa mambo yamebadilika,” alisema Sheihe Mbega na kuongeza;
“Ukiwa sheikhe wa zamani mambo yote kwenye dua,hili tujadili kwa kina mfano Sheikhe Kabeke anataka shughuli ya Allah (Mwenyezi Mungu) isonge kazi iendelee kwa sababu kumcha Mungu si kuvaa mavazi ya kisuna na kuwabeza wengine.”
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Massala, aliwapongeza watoto wa madrasa ya Jihad na namna walivyotengezwa (kufundishwa) ana kuwapitisha waislamu kwenye dini yao.
“Wamedhihirisha kuwa madrasa zinawajenga watoto kuwa wazalendo kwa nchi na dini yao,hayo yaliyowekezwa kwa watoto wetu ndio na serikali inahangaika nayo kuwekeza kwenye elimu na uzalendo,”alisema Mkuu huyo wa wilaya ya Ilemela.