WENYEJI, Manchester City wameendeleza mawindo yao ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Aston Villa 2-1 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Etihad.
Mabao ya Manchester City yalifungwa na Ruben Dias dakika ya 27 na Bernardo Silva dakika ya 43, wakati la Aston Villa lilifungwa na Ollie Watkins dakika ya 47.
Manchester City inafikisha pointi 32 baada ya ushindi huo, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Chelsea inayoongoza baada ya timu zote kucheza mechi 14, wakati Aston Villa inabaki na pointi zake 16 za mechi 14 pia katika nafasi ya 13.