NA
K-VIS BLOG, KHALFAN SAID, MBEYA
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda, amewataka madaktari wanaopatiwa mafunzo ya jinsi
ya kufanya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi (impairment
assessment of occupational accident and diseases) kufanya kazi hiyo kwa weledi
na kuzingatia maadili.
Bw.
Nzunda ameyasema hayo jijini Mbeya, wakati akifungua mafunzo ya siku tano
yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo madaktari na
watoa huduma za afya wapatao 100 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni
Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Njomba na Iringa wanashiriki.
“Watakati
wote mnapswa kuzingatia misingi mitatu wakati mkitekeleza majukumu yenu,
weledi, uadilifu na uwajibikaji,” alisema Bw. Nzunda.
Alisema
kosa lolote dogo (any slight error) litakalofanywa katika kazi ya kufanya tathmini ya ulemavu na
magonjwa yatokanayo na kazi litapelekea athari katika maisha ya watu, uchumi wa
nchi na kuhujumu Mfuko.
Aidha
alisema lengo la Serikali la kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni
kuhakikisha wafanyakazi wanapata Mafao bora tofauti na sheria ya zamani ya
fidida kwa wafanyakazi ambapo huko nyuma fidia ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa
mfanyakazi aliyepata ajali kazini au magonjwa yatokanayo na kazi ilikuwa ni
kati ya shilingi 108,000/= na 80,000/= mtawalia.
Akitoa
neno la ukaribisho, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),
Dkt. John Mduma alisema katika kuhakikisha Mfuko unafanya jukumu lake kubwa la kutoa
fidia kwa wale ambao wanapatwa na majanga wakiwa kazini ni vema tathmini
zikafanyika kwa usahihi na kwa haraka.
“Hili
la usahihi lina maanisha tunahitaji kushirikiana na wenzetu hawa ambao tayari
ni wataalamu katika maeneo hayo na hili la uharaka lina maanisha Mfuko hauwezi
kuwa na madaktari kila kona ya nchi kwa hiyo tunahitaji madaktari ambao wako
kwenye vituo hivyo kushirikiana nasi katika kuhakikiasha kwamba swala la
tathmini linafanywa kwa haraka na hivyo muhusika anapata fidia stahiki na kwa
wakati.” Alifafanua Dkt. Mduma.
Alisema
Mfuko utaendelea kufanya kazi zake kwa weledi ndiyo maana unaendelea kuwajengea
uwezo wataalamu hao wa afya.
“Tumeandaa
miongozo ili kuhakikisha kwamba tathmini zinazotolewa na wataalamu hawa
zinakuwa na uhakika, zinaaminika na zinatabirika kwa maana kwamba ziko
consistent pale ambapo ukifanyiwa tathmini na mtaalamu A na B matokeo
yasitofautiane sana.” Alifafanua.
Dkt.
Mduma aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla wake kwa jinsi
ambavyo imekuwa ikishirikiana na Mfuko katika kuhakikisha unaendelea kutoa
huduma zake kwa ufanisi zaidi.
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw.
Tixon Nzunda akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya tathmini za ulemavu
na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya Novemba 30, 2021. Mafunzo hayo
yanaratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw.
Tixon Nzunda akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya tathmini za ulemavu
na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya Novemba 30, 2021. Mafunzo hayo
yanaratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Tthmini, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF,
Dkt. John Mduma, akitoa neno la utangulizi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya tathmini.
wakisikiliza hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo.
wakisikiliza hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo.
wakisikiliza hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo.
wakisikiliza hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo.
wakisikiliza hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo.
madai, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Matilda Rusibamayila, akijibu
maswali mbalimbali ya washiriki kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko
Uhusiano na Mawasiliano, WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia) Mwenyekiti wa jopo la
wataalamu (watoa mada), Dkt. Robert Mhina (katikati), na Mtaalamu wa magonjwa
yatokanayo na kazi, Dkt. Hussein Mwanga wakijadiliana jambo.