Klabu ya Simba imeendelea kuifukuzia Yanga,Kileleni mwa msimamo baada ya kuichapa Geita Gold mabao 2-1 mchezo wa Ligi ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Peter Banda katika dakika ya 9 akimalizia pasi kutoka Kibu Denis hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja kwa bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 57 Simba walipata bao kupitia kwa kiungo Mkabaji Mzamiru Yassin.
Bao la kufutia machozi la Geita limefungwa na Mshambuliaji Juma Mahadhi dakika ya 67 na kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 17 na kubaki nafasi ya pili huku Yanga wakiwa wanaongoza wakiwa na Pointi 19.