Mwenyekiti wa kikundi cha Katavi yetu Deocredo Mlugala akikabidhi msaada
Watoto wakiwa wamekaa katika moja ya bweni la kituo hicho
……………………………………………
Na. Zillipa Joseph, Katavi
Kituo cha Gethsemani cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo katika kata ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kimeomba mchango wa hali na mali kutoka kwa watu mbalimbali wenye nia njema ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika kituo hicho kukaa katika mazingira bora zaidi.
Msimamizi wa kituo hicho Stanley Agriano ametoa ombi hilo wakati anazungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kawaida kutoka kwa wasamaria wema.
Agriano ameiomba jamii kushirikiana katika malezi ya watoto hao ambao mpaka sasa wapo 123
Wakizungumzia mchango waliotoa mara baada ya kuwatembelea watoto hao Mwenyekiti wa kikundi cha Katavi yetu Deocredo Mlugala amesema wameguswa kutoa mchango kwa ajili ya watoto
Amesema wametoa mafuta ya kupikia, mafuta ya kujipaka, sabuni, unga wa ngano, mchele, juisi na biskuti vyenye thamani ya shilingi 350,000/- kwa ajili ya watoto hao