Mmoja wa viziwi akieleza jambo katika mkutano
Bango linaloonyesha herufi kwa lugha ya alama
………………………………………………….
Na. Zillipa Joseph, Katavi
Jamii imetakiwa kutambua kuwa lugha ya alama ni lugha kama zilivyo lugha zingine na ione umuhimu wa kujifunza ili kutatua changamoto ya mawasiliano baina yao na viziwi.
Wito huo umetolewa na Mwalimu Pascal Katona wa Shule ya Msingi mchanganyiko ya Majengo iliyopo katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Mwl Katona amesema utambuzi wa lugha hiyo ya alama unasaidia kurahisisha mawasiliazo na viziwi.
Amesema katika shule hiyo wana wanafunzi saba wa ngazi tofauti ambao ni viziwi na kuongeza kuwa ufundishwaji wa lugha ya alama kwa wanafunzi wa kawaida kunaleta matumaini kwa viziwi na kupata imani kwamba lugha hiyo inakuwa.
Amesema ipo haja kwa serikali kuweka msingi wa kufundisha lugha ya alama kama somo la lazima katika shule mbalimbali hapa nchini ili kurahisisha mawasiliano pindi viziwi wanapohitaji huduma mbalimbali.
Kwa upande wake mkalimani Amani Chigona amesema kuna changamoto ya jamii kumshangaa mtu anayeongea kwa lugha ya alama.