NA
KHALFAN SAID, K-VIS BLOG, MBEYA
WAZIRI
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
kwa kuipatia vitendea kazi (computers) Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili
kuharakisha shughuli za usuluhishi wa migogoro ya kikazi.
Pongezi
hizo zimetolewa na Mhe. Waziri Jenista wakati akikabidhi computer 10 kwa Mkurugenzi
Mkuu wa CMA, Bw.Shanes Nungu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mfumo wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
jijini Mbeya Novemba 29, 2021.
“Tunashuhudia
hapa Workers Compensation Fund (Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi) unakwenda
kufanya kazi nzuri ya kuiwezesha CMA ili itekeleze majukumu yake sawasawa jambo
hili ni zuri sana.” Alifafanua Mhe. Waziri.
Kipekee
napenda kuwashukuru sana sana wakuu wote na viongozi wa taasisi zote Dkt. John
Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na kaka yangu Nungu Mkurugenzi Mkuu wa CMA kwa
kuona umuhimu wa kufanya kazi kama serikali moja, ninyi wote mko chini ya
umbrella (mwamvuli) mmoja, ili kuhakikisha kwamba mmoja anapogundua changamoto
ya mwenzake anaamua kusimama naye na kuweza kumsaidia, Alisisitiza Mhe. Waziri
Jenista Mhagama
Akieleza
zaidi, Mhe. Waziri alisema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa ukifanya
vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake tangu uanzishwe miaka sita iliyopita, sheria iliyokuwepo kabla ya kupata uhuru, mfanyakazi alikuwa akiumia analipwa shilingi 108,000/= haijalishi awe amepata ulemavu wa aina gani malipo ya fidia yalikuwa ni flat rate.
“Mwaka
2008 Sheria ilifanyiwa marekebisho ambapo mwaka 2015 tuliunda Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi ambao umechukua jukumu la Fidia, kuhangaika na magonjwa na
madhara yatokanayo na kazi kutoka kwa waajiri na kuwekwa kwenye Mfumo maalum na
sasa uko kwenye Mfuko wa WCF.” Alibainisha.
Alisema
katika muktadha huo huo wa kuhakikisha serikali inayagawa majukumu kiutendaji
na kisheria ilianzisha CMA ili taasisi hii ishughulike na masuala ya usuluhishi
na uamuzi inapotekea migogoro ndani ya maeneo ya kazi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John
Mduma alisema, makabidhiano hayo ya computer ni utekelezaji wa maagizo ya
Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama aliyetaka taasisi hizo zifanye kazi kama
ndugu.
“Kwa
kufanya kazi kwa pamoja ndipo tunaweza kufikia malengo yetu kama taasisi lakini
kwa pamoja kama ofisi yako Mheshimiwa Waziri, tunatambua kwamba mmoja wetu kama
atakimbia mbio na uwezo wake alionao na akawaacha ndugu zake nyuma “hatatoboa
yeye peke yake”. Alisema Dkt. Mduma.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu alimshukuru Waziri Jenista kwa maono
yake na kuwezesha CMA kupata msada huo wa computer.
“Mheshimiwa
Waziri nakumbuka ulisema nyie watoto sita kwanza shikamaneni halafu saidianeni
na agizo lako limezaa matunda, sio mara ya kwanza kwa WCF kutusaidia mara ya
kwanza walitusaidia computer kumi ambazo zilisaidia kutatua malalamiko ya
wananchi kucheleweshewa hukumu zao kupungua.” Alishukuru Bw. Nungu.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu,
Bunge) Bw. Kspar Muya, wakurugenzi wa WCFna CMA pamoja na watumishi wa taasisi
zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni NSSF, PSSSF, OSHA na Idara ya
Kazi.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mfawidhi wa CMA jijini Mbeya, Bw. Mwangata Makawa akitoa neno la shukrani
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa CMA
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Kazi, Mbeya
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa OSHA
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF.