**********************
Samwel Mtuwa na Tito Mselem – Mwanza.
Leo Novemba 27, 2021, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzani (GST) imetoa mafunzo maalum juu ya namna bora ya uchukuaji wa sampuli wakilishi katika sehemu zao za kazi.
Mafunzo haya ya siku tano yamefunguliwa na Waziri wa Madini Doto Biteko ikiwa ni moja ya sehemu ya mpango mkakati wa kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo wa madini nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Waziri Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia yote yatakayo tolewa na wataalam wa *GST* ili waweze kupata uelewa mkubwa na kufanya Uchimbaji na uchukuaji Sampuli kwa weledi utakao saidia katika kazi zao.
Aidha Waziri Biteko amewataka wachimbaji wadogo kufanyakazi kwa umoja wa kuungana ili kuweka nguvu kubwa katika kuendeleza Sekta ya Madini kwani wachimbaji wadogo wanamchango mkubwa katika kukuza seykta ya Madini nchini.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt Mussa Budeba amewaomba wachimbaji wadogo wa madini kufuatilia kwa makini mada zote zitakatolewa na na wataalam wa *GST* ambapo watafundisha kwa namna mbili yaani nadharia na vitendo.
Sambamba na hilo Waziri Biteko ametembelea Soko la Kimataifa la Madini-Mwanza ambapo amekutana na wafanyabiashara wa madini ili kusikiliza kero zao na kuzitolea ufumbuzi pia, amewapongeza wafanyabiashara hao kwa kuhamia katika soko jipya la madini lilloipo katika eneo la Sabasaba ndani ya kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Matals Gold Refinary.