*****************************
– Afanya kikao Na Watendaji wa Mitaa Na Kata kuomba kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi.
– Maadhimisho ya kwanza ya sherehe za Uhuru kwa awamu ya sita.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla* ametoa wito kwa Wananchi *kujitokeza kwa wingi* kwenye Sherehe za Maadhimisho ya *Miaka 60 ya Uhuru* zinazotaraji kufanyika *Disemba 09* kwenye *Uwanja wa Uhuru.*
*RC Makalla* ametoa wito huo wakati wa *kikao Cha pamoja na Watendaji wa Kata na Mitaa* kilichoketi leo kuweka mikakati ya *Maandalizi ya Sherehe* hizo ambazo zitakuwa za kwanza kwa *Serikali ya awamu ya sita* Chini ya *Rais Samia Suluhu Hassan.*
Aidha katikati kuelekea Sherehe hizo zitatanguluwa na uzinduzi wa *Miradi mbalimbali ya maendeleo.*
*Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zitahudhuriwa na Wakuu wa Nchi mbalimbali watakaowasili nchini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Tanzania.*