Mkuu wa Kitengo cha Elimu Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani SP Mossi Boniface Ndozero akiwafundisha wanafunzi toka Shule ya Msingi Meru Primary School jinsi ya kuvuka na kuvusha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, Mafunzo hayo yanatolewa maeneo mbalimbali katika jiji la Arusha ambapo Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yanayofanyika Kitaifa mkoani humo.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani SP Mossi Boniface Ndozero akionyesha mfano wa Ubebaji usio salama kwa wanafunzi kwenye pikipiki Mafunzo hayo yamefanyika katika shule ya Msingi Meru Primary School.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Khamis Hamza Chilo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Lush iliyopo mkoani Arusha kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa. (Picha na Jeshi la Polisi)