Watumishi wa chuo cha afya cha St Maximiliancolbe mjini Tabora wakiwa na mwakilishi wamkoa wa Tabora Msalika Makungu aliyekaa katikati akiwa na suti nyeusi aliyekaa kulia kwake ni mkurungezi wa chuo hicho Elizabeth Nkonyoka aliyefaa tisht Nyeupi na aliyekaa wapili kutoka kushoto ni mkuu wa chuo cha afya Nassoro Madende
wanachuo wakisubiri kufanyiwa vipimo vya afya
…………………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewakata watanzania kuwekeza mkoani hapa kutokana na kuwepo kwa fursa mbali mbali katika nyanja za biashara ,elimu na ufugaji lengo ni kuinua uchumi wa mkoa
Wito huo ulitolewa jana na mkuu huyo katika hotuba yake iliyosomwa niamba yake na Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati akizindua utoaji wa huduma za afya bure kwa jamii katika chuo cha afya cha St Maximiliancolbe mjini Tabora.
Alisema kwamba mkoa huo umebarikiwa kuwa na rasilmali nyingi ambazo zinaitaji wawekezeji kutoka Tanzania na nje ya Tanzania .
Balozi Dkt. Batilda Buriani alisisitiza kwamba kuwekeza kwenye elimu ,kilimo cha mazao mbalimbali na mazao ya nyuki ambayo bado ya nanafasi kubwa kwenye uchumi wa dunia kwa sasa.
Alisema kwamba kwenye mkoa huo Fursa Zipo Nyingine ambazo zinaweze kuwanufaisha wakazi wa mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani ambazo zitanufaika kwa ujio wa wawekezaji hao mkoani hapa.
Alisema licha ya kuwezeka mkoani hapa pia kupita kwa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi mkoani Tanga litawanufaisha wananchi wengi kiuchumi kuanzia wafanyabiashara wadogo wakati na wale wakubwa .
Katika hatua nyingine mkuu wamkoa wa Tabora amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kutumia fursa ya matibabu bure iliyotolewa na chuo cha Maximiliancolbe kufanya uchunguzi wa afya zao pamoja na kushiriki zoezi la kuchangia damu.
Awali akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora,Mkuu wa Chuo cha ST Maximiliancolbe,Nasoro Madende alimuomba Kiongozi huyo kuona namna ambavyo serikali inawezesha kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vya kati kufikia ndoto zao katika elimu kwa kuwakopesha fedha au kuwatafutia wafadhili.