Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kimataifa ya kuuza magari ya BE FORWARD ,Daniel Japhet akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusiana na huduma wanazotoa.
Mwenyekiti wa wamiliki wa malori wadogo na wa kati (TAMSTOA),Chuki Shabani akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Waliopo pichani ni wafanyakazi wa kampuni ya BE FORWARD yenye makao yake makuu jijini Dar es Saalamu wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao jijini Arusha .
……………………………………………………
Happy Lazaro,Arusha.
Watumiaji wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kutii sheria bila shuruti ili kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipoteza nguvu kazi iliyo nyingi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kimataifa ya uuzaji wa magari ya BE FORWARD yenye makao yake makuu jijini Dar es Saalam,Daniel Japhet wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda lao katika uwanja wa Stadium jijini Arusha.
Amesema kuwa,endapo watumiaji wa barabara watatii sheria bila shuruti itapunguza Sana ajali zinazoweza kuepukika .
“Sisi Kama wadau wa kuuza magari Tanzania tunahamasisha watumiaji kutii sheria na kufuatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuzitumia bidhaa zetu kwani zina ubora wa hali ya juu na huo ndo ukweli na uwazi sisi hatuna biashara ya longolongo tunajiamini kwa kile tunachokifanya.”amesema Daniel.
Daniel amesema kuwa,wao kama wauzaji wa magari Tanzania wameona watoe sehemu ya faida yao kwa ajili ya kuja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto katika kuwahamasisha kufuatia sheria na kanuni ili kuepukika kwa ajali.
“Tumekuwa tukitengeneza wastani wa magari elfu nane hadi elfu kumi kwa mwezi ambapo tumekuwa tukitumia bandari ya Dar es Saalamu Zambia na Malawi, hivyo tunawaomba Sana wananchi wajitokeze kwa wingi kutuunga mkono kwa kununua bidhaa zetu kwani ni za uhakika na Zina ubora wa hali ya juu.”amesema Daniel.
Naye Mwenyekiti wa wamiliki wa malori wadogo na wa kati,(TAMSTOA)Chuki Shabani alisema kuwa chama hicho kipo Kama ngazi kati ya serikali na wanachama katika kushirikiana kutoa elimu kwa wafanyabiashara wasafirishaji wa malori juu ya umuhimu wao katika kufuata sheria .
Amesema kuwa, madereva malori wamekuwa wakisoma mara kwa mara kwa ajili ya kujikumbusha jinsi ya kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani na kuepukana na ajali za mara kwa Mara.