MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe,akionyesha miradi yote kwa ajili ya ukarabati wa barabara katika Mkoa wa Dodoma ambazo zitagharimu shilingi bilioni 48.97 wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja Mstaafu Johnick Risasi,akichagia hoja wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akishuhudia utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe,akimkabidhi Mkataba Mkurugenzi Mkuu kutoka Kampuni ya Chenjela Mhandisi Agnes Shawa wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amewataka wakandarasi waliopewa miradi ya barabara katika Mkoa wa Dodoma kuifanya kwa kiwango kizuri ili waweze kuaminiwa kwa mara nyingine.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara,Mtaka amesema bajeti ya Mkoa wa Dodoma ni sawa na Mikoa mitano hivyo wakandarasi hao wanatakiwa kufanya kazi ya kueleweka ili kazi nyingine inapotokea waweze kuaminiwa.
“Nawaambia wakandarasi hii bajeti tuliyonayo hapa ni ya Mikoa mitano kaa hapa fanya kazi ili upate kazi nyingine. Juzi nimeenda Donbosco wanaeneo pale likifika wakati wa mvua mtihani kule Nkuhungu kuna shule inajengwa wakati wa mvua kuna shida kubwa.Mimi natamani tuende kufanya miradi mizuri,”amesema.
Vilevile,amesema wamesaini mkataba huo kwa upendo jambo ambalo ni jema lakini baada ya miezi mitatu hali huwa tofauti kwani upendo huo hugeuka na kuwa chuki.
“Tumekuja kwenye jambo jema kusaini sasa inaleta shida sana nyinyi mmetualiaka kwa upendo halafu baada ya miezi mitatu huu upendo unageuka na kuwa chuki,kesho Takukuru anageuka anawaweka ndani jambo hili linaniumiza.
“Tumeitana hapa baada ya miezi mitatu hali inakuwa mbaya tumekuja kushuhudia jambo jema .Ndio maana wakandarasi wa Tanzania hatukui kwa sababu ya ubabaishaji matarajio yangu anaefanya kazi kwa milioni 40 focus yake ni bilioni 1.
“Kusaini sio shida haya si makaratasi tu lakini kwa kiwango gani ambacho yaani kuna mtu amejenga vumbi bado hajaweza kumaliza km 100,Lakini ni taabu taabu kwenye hii ya leo mimi nawapongeza CRDB kuna vitu ambavyo Benki tukiendelea kuwekeza tutasainia miradi yetu.
“Tuna madeiwaka kwenye mabodaboda kwenye bajaji,basi fuso,ukandarasi tarura,”amesema.
Aidha,Mtaka amesema kunahaja ya wafanyakazi wa Serikali kuwajibu vizuri wateja wanaokuja ofsini.
“Hapa Dodoma anaweza akaja mtu kumbe ni ofisa mwenzako mjibu mtu vizuri anapokuja ofsini kwako ukikubali kuwa mnyama wa kazi za Serikali wala usikwaze watu ndio kazi yako,”amesema.
Pia Mtaka amesema anatamani kuona wakandarasi wanawake wanaongezeka katika ujenzi wa barabara na majengo.
“Ningetamani kuona wakandarasi wanawake sijui tutafanyaje kwa sababu kazi zipo Tanroad yale magroup ya whatsup tuma miradi ili watu waombe sasa wanawake wamepata wangapi katika wanadarasi 29,”amesema.
Kwa upande wake,Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe,amesema miradi yote kwa ajili ya ukarabati wa barabara katika Mkoa wa Dodoma itagharimu shilingi bilioni 48.97.
Amesema kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuna matengenezo ya barabara ya Kisasa,Itega, Njendengwa na Dodoma town pamoja na uzibaji wa viraka na uwekazi wa alama za barabarani ambapo jumla ni shilingi bilioni 193.492
Pia amesema kuna matengenezo ya barabara katika maeneo ya Ndejengwa na Itega kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi ambapo amedai wametenga milioni 58.9 kwa ajili ya matengenezo hayo.
Vilevile amesema kwa upande wa Bahi zimetengwa shilingi milioni 948.264 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Mwitikira na Mtitaa kwa kiwango cha Changarawe.
Amesema kwa upande wa Halmashauri ya Chamwino kutakuwa na miradi mitatu ya kutengeneza barabara yenye thamani ya shilingi bilioni 3.36.
Amesema kwa upande wa Kongwa jumla ya miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.09 itatekelezwa na kuna miradi ya kutengeneza barabara kwa nguvu kazi thamani yake ni milioni 40 pamoja na matengenezo ya kawaida Mtanana,Makawa kwa kutumia vikundi maalum.
Naye,Meneja wa Tarura Wilaya ya Mpwapwa,Mhandisi Emanuel Lukumay amesema wametia saini mkataba wa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami kilomita moja Kibakwa na moja Mpwapwa Mjini pamoja na ujenzi wa vivuko na barabara za changarawe.
“Kikubwa kama alivyosema Mkuu wa Mkoa Wakandarasi wajitahidi wakafanye kazi zenye tija kwa watanzania,”amesema