Mnamo tarehe 22.11.2021 majira ya saa 05:00 Asubuhi huko maeneo ya Matundasi, Mji Mdogo wa Makongolosi, Mkoa wa mbeya. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliendesha msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa aliyehusika katika tukio la mauaji ya ADAM JACOB [31] mchimbaji, mkazi wa kitongoji cha Kasakalawe na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa DEVI ABRAHAM MWAMBEBULE @ SKACHA [32] Mkazi wa Matundasi. Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kuhusika katika tukio hilo. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Imetolewa na.
ULRICH MATEI – SACP
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,