VINARA, Chelsea wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa King Power.
Mabao ya The Blues yamefungwa na Antonio Rudiger dakika ya 14, N’Golo Kante dakika ya 28 na Christian Pulisic dakika ya 71 na kwa ushidi huo, Chelsea inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 12 na sasa wanawazidi pointi sita Manchester City wanaofuatia ambao pia wana mechi moja mkononi.
Leicester City inabaki na pointi zake 15 za mechi 12 katika nafasi ya 12.