Mhandishi Naomi Mcharo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akionesha maeneo ya hifadhi yanayozunguka bwawa la Dongobeshi hayapo katika picha. |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Mji Bw. Faustine
Masunga, akizungumza kuhusu faida zitokanazo na kilimo cha Umwagiliaji
alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake mwishoni mwa
wiki.
Picha Ikionesha Bwawa la Dongobeshi linalotumika katika shughuli za
kilimo cha umwagiliaji likiwa katika hali ya upungufu wa maji.
Na; Mwandishi wetu – Manyara.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi Calorina Mtapula, ametoa wito kwa wakulima
wa kilimo cha umwagiliaji Mkoani humo, kutoa tozo na ada zilizopo
kisheria katika kilimo cha umwagiliaji, ili kuweza kuchangia maendeleo
ya sekta hiyo nchini.
Ameyasema
hayo Mkoani Manyara Mwishoni mwa wiki, alipokuwa akizungumza na timu ya
watumishi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na waandishi wa Habari
iliyopo Mkoani humo katika kampeni maaalum ya kutoa elimu kwa watendaji
na wakulima kuhusiana na swala zima za utoaji wa ada na tozo za
umwagiliaji kwa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji nchini.
Katibu Tawala huyo, amewataka wakulima kulibeba jambo hili na kulifanyia kazi na kusema kuwa ni kwa manufaa yao wenyewe.
“Wakulima
tujiunge kwenye vikundi ili tuwezi kuwepo katika skimu na kuweza kupata
mavuno na kutoa ada na tozo ambazo zinarudi kwa wakulima wenyewe.”
Alisema
Sambamba
na hilo Bi Calorie Mtapula, ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri
zote za Mkoa wa Manyara kusimamia kwa kila hali zoezi hilo na
kuhakikisha wakulima wanatoa ada na tozo hizo na kuwekwa kwenye mfuko wa
maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji. “Isije kutokea 75% ya ada na tozo
inayobakia kwa wakulima ikanufaisha watu wachache kwa maslahi yao
Binafsi.” Alisisitiza.
Kwa
Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Babati Mji Bw. Faustine Masunga amesema
kuwa, wana jukumu la kuelimisha wananchi na waelewe majukumu yao kama
wananchi kwenye swala zima la kilimo cha Umwagiliaji kwani linalenga
kupunguza njaa na kuongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja pato la
Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Akiongea
wakati timu hiyo ilipotembelea bwawa la Dongobesh, Mhandisi Naomi
Mcharo kutoka Tume ya taifa ya Umwagiliaji alisema kuwa Kilimo cha
Umwagiliaji ni njia pekee ya kukabiliana na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabianchi , kwani kwa sasa nchi imeingia katika kipindi
kirefu cha ukame kilichopelekea upungufu wa maji na mvua.
Amewaasa
wanachi wanaozunguka bwawa hilo linalotumika katika shughuli za kilimo,
kuachana na shughuli nyingine za kibinadamu katika chanzo hicho na
kutunza na kuhifadhi mazingira.
Mhandisi
Naomi Mcharo, alisema Tume ya Taifa ya uwagiliaji imejipanga
kikamilifu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kumuwezesha
mkulima kutumia maji kwa uangalifu, kutumia maji kidogo na kuzalisha
zaidi bila kututegemea mvua ambayo kwa sasa imekuwa ni changamoto.
Tume
ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kutoa elimu ya tozo na ada za
umwagilia kwa watendaji na wakulima kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara