********************
Na.Samwel Mtuwa – Manyara
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) yaendelea kufanya Utafiti wa jiosayansi mkoani Manyara katika wilaya ya Kiteto.
Kufanyika kwa Utafiti huu wa awali ni sehemu ya mpango wa utekelezaji wa majukumu yake kama ilivyojipangia.
Katika kuhakikisha Utafiti unafanyika kwa ufasaha zaidi ya wataalam 40 wa jiosayansi wamefanikiwa kuchukua zaidi ya sampuli *1000* za Miamba katika vijiji mbalimbali vilivyopo katika Quarter Degree Sheet *(QDS)* namba *125* na *126* ili kuzifanyia Uchunguzi wa Maabara.
Tafiti hizi za awali zinazofanywa na *GST* zina lengo la kuibua maeneo mapya yenye uwepo wa rasilimali Madini ili kuendeleza sekta ya madini nchini.
Akizungumza katika eneo la Utafiti Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia *GST* Dkt. Ronald Massawe , amesema kuwa katika Utafiti huu wa awali wataalam wamefanikiwa kupata sampuli nyingi zitakazo saidia kubaini viashiria vya uwepo wa madini kama vile Madini ya chokaa.
Utafiti huu wa awali mkoani Manyara umetumia zaidi ya muda mwezi mmoja katika upimaji na uchukuaji wa sampuli.
*Zifuatazo ni baadhi ya picha za wataalam wakiwa katika eneo la ugani wakichukua na kupima sampuli za Miamba*