**********************
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mpaka sasa Wananchi waliojiunga na Bima ya Afya Nchini ni asilimia 14 tu huku wananchi huku asilimia 86% ya Watanzania wakiwa wanalipia huduma za matibabu kwa kutoa hela mfukoni pale wanapougua.
Hii maana yake ni kwamba Watanzania hawa wanapata changamoto pale ambapo wanapata maradhi na wakti huo hawana fedha mfukoni au hawapati huduma stahiki kwa sababu hawana fedha ya kutosha kupata huduma hiyo kwa muda huo.
Lakini pia wananchi hao mara nyingi wanapata changamoto ya kuingia katika umaskini kwa sababu ya kugharamia matibabu kila wanapougua.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Jijini Arusha Dkt. Grace amesema haijalishi unajiunga na bima gani cha msingi kila mwananchi awe na Bima ya Afya.
Dkt. Grace ameongeza kwa tathmini ya haraka nimegundua kuwa watu wengi hawana uelewa wa masuala ya Bima ya Afya lakini wengi wao wana uwezo wa kulipa.
Kufuatia hali hiyo nizitake kamati za Afya Mikoa na Wilaya(RHMT&CHMT) kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha katika kila ngazi ili kuwafikia wananchi wengi zaidi kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya.
Wananchi wakielimishwa vizuri watajiunga na Bima ya Afya yeyote ili kuondokana na adha wanayoipata pale wanapopata maradhi kwa kushindwa kugharamia matibabu na kusababisha madeni , umaskini na pengine kifo.