Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji wa Vodacom George Lugata (kulia) na Meneja Msaidizi wa Carl Care walipokuwa wakizindua huduma hiyo kwenye duka la Vodacom Mlimacity, Dar.
*****************************
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom PLC na Kampuni ya Carl Care leo wamezindua huduma ya pamoja ya kukarabati simu za wateja wa Vodacom ambazo wamezinunu kwenye maduka ya Vodacom yaliyopo zaidi ya 450 hapa nchini.
Akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi huo uliofanyika duka la Vodacom lililopo Mlimani City, jijini Dar, leo Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom George Lugata amesema wameamua kushirikiana na Carl Care kwa ajili ya kuondoa changamoto zinazowakabili wateja mbalimbali wa simu.
“Wateja mbalimbali wa simu za mkononi wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali kwenye matumizi ya simu zao lakini sisi kama Vodacom tumeamua kushirikiana na Carl Care kuondoia tatizo hilo kwa watumia wa simu zetu ambazo wamezinunua kwenye maduka yetu.
“Simu zetu zinazohusika katika mpango huo ni TECNO, Ifinix na Itel ambazo zimenunuliwa kwenye maduka yetu”.
“Miongoni mwa maduka yetu yaliyopo sehemu mbalimbali hapa nchini ni pamoja na Mbeya, Arusha, Shinganya, Morogoro, Dodoma, Geita, Songea na kwingineko.
Katika jiji la Dar es Salaam tuna maduka kadhaa ikiwemo duka la Makao Makuu ya Vodacom pale Morocco, Mlimani City, Msimbazi na lile la Mtaa wa Samora” alisema Lugata.
Lugata amewashauri wateja wa Vodacom wanaotaka kujua zaidi kuhusu huduma hiyo kuingia kwenye website yao ambapo watajionea zaidi kuhusu huduma hiyo na nyinginezo.
Naye Meneja Msaidizi wa Carl Care, Winniel Michael amesema kampuni itahakikisha inatoa huduma bora wateja watakaokwenda kupata huduma hiyo wakiwatumia mafundi wao wenye uzoefu pamoja na kuweka vifaa orijino kwenye zitakazopelekwa kufanyiwa ukarabati.