Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akizindua kitabu cha Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha kwa njia ya kidijitali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyagasa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akifurahia baada ya kuzindua kitabu Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha kwa njia ya kidijitali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyagasa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akiwa amezindua kitabu cha Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha kwa njia ya kidijitali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyagasa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, ambapo alisisitiza utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kamishana Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Deoninsia Mjema akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na wizara hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, alipotembelea banda hilo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Benard Kibesse baada ya uzinduzia wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha Kamishana Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Deoninsia Mjema kwa niaba ya wizara hiyo baada ya uzinduzia wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mpango wa Taif awa Elimu ya Fedha Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Zanzibar, Bw. Kamal Muhsin Ramzar baada ya uzinduzia wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyagasa, kushoto ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja.
(Picha Josephine Majura, WFM, Dar es Salaam)
****************************
Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, amewaagiza washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za fedha Kitaifa kujikita katika kutoa elimu ya huduma za fedha ambazo ni rahisi kutumiwa kwa Watanzania zenye lengo la kuongeza kipato na kupunguza umaskini wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Waziri Jamal Kassim Ali ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam yaliyoanza Novemba 8 na kutarajiwa kuhitimishwa Novemba 14 mwaka huu.
Alisema kuwa moja ya sekta ambazo Serikali imekuwa ikiziboresha mara kwa mara ni Sekta ya Fedha ambapo kwa zaidi ya miaka ishirini Sekta ya Fedha imekuwa ikiboreshwa ili kuwezesha Watanzania kuhudumiwa ipasavyo kwa lengo la kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na kupunguza au kuondoa kabisa Umaskini kwa Watanzania.
“Hatuwezi kukabilia na changamoto za huduma za fedha bila kuwa wabunifu ili kuweza kuongeza kipato, wigo wa kulipa kodi na kuchangia katika maendeleo ya Taifa”, alisema Mhe. Jamal Kassim Ali.
Aidha alisema mafanikio yaliyopatikana kutokana na uboreshaji wa Sekta ya Fedha uliofanywa na Serikali ni kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa kwa asilimia 3.1 kwa mwaka 2020, kuimarisha huduma za kifedha kwa wananchi kutokana na kutungwa kwa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019 pamoja na kuboresha usimamizi wa taasisi za fedha na maadili ya watumishi wa taasisi hizo ili kumlinda mteja.
Kwa upande wake Kamishna wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini Dkt. Charles Mwamwaja, alisema kuwa Serikali imeanzisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha 2021/22 hadi 2029/2030 na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (5) wa Elimu ya Fedha (2019/20 hadi 2025/26).
Alisema watanzania chini ya asilimia 50 ndio waliofikiwa na huduma za fedha jambo ambalo limeifanya Serikali kuwa na Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ili kuongeza uelewa kwa wananchi kwa lengo la kuchochea ustawi wa jamii.
Dkt. Mwamwaja alisema kuwa washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ni pamoja na Benki, Taasisi za Bima, Masoko ya Mitaji na Dhamana, Mifuko ya Jamii na Huduma ndogo ya Fedha.
Akielezea maendeleo ya Sekta ya Fedha yaliyofikiwa nchini, Dkt. Mwamwaja aklisema kuwa Maboresho yalifanyika katika Sekta Fedha yameleta mafanikio kwa upande wa sekta binafsi ambapo mikopo kwa sekta hiyo ilikua kwa asilimia 4.1, uwiano wa mikopo chechefu ulikuwa asilimia 9.30 hadi kufikia juni, 2021 ambao ni juu ya kiwango kinachokubalika na Benki cha asilimia 5.
Alisema kuwa riba za mikopo zilifikia asilimia 16.60 kwa mwaka ulioishia Juni, 2021 na faida katika Sekta ya benki kabla ya kodi kwa wastani wa mali ilikuwa asilimia 2.42 mwezi Juni, 2021 na uwiano wa faida baada ya kodi kwa wastani wa fedha za wanahisa uliongezeka kufikia asilimia 10.47 mwezi Juni, 2021.
Katika hafla ya kufungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa Nchini, kumezinduliwa Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2025/26.