Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, akifungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, yanayofanyika jijini Mwanza.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mwanza, Mhandisi Boniface Mkumbo, akisoma taarifa yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana (hayupo pichani), kuhusu Semina ya Mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, yanayofanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi, (aliyefunga kitambaa cha pinki), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa usafirishaji katika Semina ya Mafunzo kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 yanayofanyika jijini Mwanza.
Mtaalamu Kitengo cha Mizani kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Vicent Tarmo, akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya usafirishaji, kuhusu ya Sheria ya Afrika Mashariki ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo ya kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yanayofanyika jijini Mwanza
Picha na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi