Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akishiriki zoezi la uwekaji zege la chini kwenye msingi wa mojawapo ya daraja linalojengwa kati ya Madaraja 21.
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akishiriki kujenga kwenye kituo cha Afya cha Tarafa ya Mihambwe alipofanya ziara kujionea maendeleo ya mradi. Pembeni ni mojawapo ya fundi saidia akifuatiwa na Mwenyekiti Kamati ya ujenzi mradi huo.
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akikoroga zege pamoja na mafundi kwa ajili ya kumwagwa kwenye msingi wa darasa linalojengwa
******************************
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu leo Novemba 8, 2021 ameendelea na ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi miradi ya kimaendeleo.
Gavana Shilatu ametembelea miradi ya ujenzi ya kituo cha Afya cha Tarafa ya Mihambwe, vyumba vya Madarasa shule za Sekondari na shule shikizi inayooendelea kujengwa ndani ya Tarafa ya Mihambwe na huku akisisitiza kasi ya ujenzi iongezwe huku ubora na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha ya mradi husika uzingatiwe.
“Tarafa ya Mihambwe tulisha puliza kipyenga cha ujenzi. Nahitaji kuona kasi, ubora na viwango vikizingatiwa kwenye miradi yote ya kimaendeleo. Tunataka ifikapo mwishoni wa mwezi huu Novemba ndani ya Tarafa ya Mihambwe tumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kazi aliyotutuma ya ujenzi huu ikiwa imekamilika vyema. Kwahiyo tujitume vilivyo ikamilike kwa wakati.” Alisisitiza Gavana Shilatu.
Tarafa ya Mihambwe imepata fedha Tsh. Milioni 250 (Tsh. 250,000,000/=) za tozo ya miamala ya simu za kujenga kituo cha Afya Mihambwe na Tsh. Milioni 420 (Tsh. 420,000,000/=) kujenga Madarasa 21 fedha za mkopo nafuu za kupambana na Uviko 19 kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Taifa.