******************************
WATU WATANO (5) WA FAMILIA MOJA WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA AJALI YA MOTO KUUNGUZA NYUMBA, HUKO BARABARA YA TWIGA, MTAA WA IGOMA MASHARIKI, KATA YA IGOMA, WILAYA YA NYAMAGANA. WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO YA MOTO NI LAMECK BENEDICTO, MIAKA 32, MSUKUMA, MWENDESHA BODABODA, MKAZI WA IGOMA, MKEWE AITWAYE LEYAH LAMECK, MIAKA 26, MKULIMA, MKAZI WA IGOMA MASHARIKI, MTOTO WAO YUNITH LAMECK, MWAKA 01, NA VIJANA WAWILI WAKIUME MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA AMBAO WALIMTEMBELEA HAPO JANA TAREHE 07/11/2021.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 08/11/2021 MAJIRA YA SAA 00:05 USIKU MAENEO TAJWA HAPO JUU, HII NI BAADA YA NYUMBA NAMBA 21 MALI YA JAMASON SALUMU @ MBONABUCHA, MIAKA 41, MUHA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MBUGANI KATA YA KISHIRI, ILIYOJENGWA KWA TOFARI ZA SARUJI NA KUEZEKWA KWA BATI NA KUUNGANISHWA UMEME WA TANESCO IKIWA NA WAPANGAJI WANNE NDIPO CHUMBA NA SEBURE CHA MPANGAJI LAMECK BENEDICTO AMBAYE NI MAREHEMU KWA SASA GHAFLA KILIWAKA MOTO NA KUTEKETEA NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO KINACHUNGUZWA, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU- TOURE KUSUBIRI UCHUNGUZI WA DAKTARI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI. THAMANI YA MALI ZILIZOTEKETEA KATIKA AJALI HIYO BADO HAZIJAJULIKANA. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO.