Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA umefanya kikao na Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kuboresha namna ya ushiriki wa kuzuia na kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia hususani wanawake na watoto.
Akizungumza leo Jumamosi Novemba 6,2021 wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Nitesh Manispaa ya Kahama,Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija amesema nia kuu ni kuchochea njia bora za kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia hasa yanayowakumba wanawake na watoto ili kuongeza ustawi wa wanawake na watoto katika jamii.
“Kikao hiki kinacholenga kujadili mafanikio,changamoto, kujifunza na mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA tangu mwezi Julai 2020 katika kata za Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala. Tunataka tupate matokeo chanya ili kuwapatia haki waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia”,amesema Shija.
Shija ametumia fursa hiyo kuwataka Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya taarifa na maarifa kutoa rufaa kwa kesi za migogoro ya ardhi na ndoa badala ya kukaa nazo.
“Kuna kesi ambazo hupaswi kuzisuluhisha bali zipelekwe ngazi zinazotakiwa. Usihangaike na jambo ambalo huhusiki nalo, mfano migogoro ya ndoa na ardhi ipelekwe kwenye mamlaka zingine, msiwe kama baadhi ya maafisa watendaji ambao wanakaa na kesi hizo. Usikae na kesi isiyokuhusu, kama imekushinda kabisa achana nayo”,amesema Shija.
Aidha amefafanua kuwa Mahakama ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuvunja ndoa na kugawanya mali za wanandoa hivyo kuwataka baadhi ya viongozi ngazi za vijiji, mitaa, vitongoji, kata wakiwemo maafisa watendaji kuacha tabia ya kusuluhisha kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji, mimba na ndoa za utotoni.
Hata hivyo amesema Wasaidizi wa Kisheria wana wajibu wa kutoa ushauri wa kisheria kwa wana vituo vya taarifa na maarifa kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia na wana vituo vya taarifa na maarifa kuomba ushauri pindi wanapokutana na changamoto katika kushughulikia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Nao washiriki wa kikao hicho akiwemo Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya, Loyce Kabanza na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Lameck Manyesha wamesema wananchi wameanza kuachana na baadhi ya mila na desturi zisizofaa mfano Wacheza ngoma ya Ukango ambao sasa wamepunguza matumizi ya matusi wanapocheza ngoma zao.
Kwa upande wao, Wasaidizi wa Kisheria Phillip Jackson Sesawanga na Jacob Paul Nyalulu wamesema bado kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanapoteza ushahidi wa matukio ya ukatili wa kijinsia hali inayokwamisha kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Lakini pia bado wananchi wanakumbatia matukio ya ukatili,baadhi ya wanawake wakibakwa hawatoi ushirikiano kwa kutoa ushahidi, wanaume nao wanafanyiwa ukatili wa kijinsia mfano kupigwa lakini hawasemi, wanaona aibu kusema na bado kuna wazazi wanawataka watoto wao kufeli kwenye mitihani ili waolewe”,amesema Sesawanga.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA leo Jumamosi Novemba 6,2021 katika ukumbi wa Nitesh Manispaa ya Kahama. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya, Loyce Kabanza akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Lameck Manyesha akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Msaidizi wa Kisheria David Mlyandili akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Msaidizi wa Kisheria Phillip Jackson Sesawanga akichangia hoja kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA.
Mwana kituo cha taarifa na maarifa kutoka kata ya Lunguya Gaudensia Macheye akichangia hoja kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog