Meneja wa shule za New life primary na New life Olosiva Sekondari zinazomilikiwa na shirika la New Life outreach , Nicodemus Tagara akizungumza shuleni hapo.(Happy Lazaro).
**************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Wazazi kwa kushirikiana na walezi wametakiwa kutoa motisha kwa watoto wao kwa kuwaendeleza kitaaluma kwani ndio urithi pekee wa kuwapatia ili waweze kufikia ndoto zao walizojiwekea.
Hayo yamesemwa na Meneja wa shule ya msingi New life na shule ya Sekondari ya New life Olosiva zinazomilikiwa na shirika la New life outreach lililopo kata ya Olorieni ,Nicodemus Tagara wakati akizungumza katika mahafali ya darasa la Saba na kidato cha nne shuleni hapo.
Amesema kuwa, watoto wengi wamekuwa na malengo makubwa ya kufika mbali ila changamoto kubwa imekuwepo kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwakatisha tamaa watoto wao kwa kushindwa kuwaendeleza ili kufikia ndoto zao,hivyo amewataka kutowakatisha tamaa ili watoto hao watimize ndoto zao.
Amesema kuwa,shule hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa cha ufaulu ambapo ufaulu huo umekuwa ukipanda kila mwaka kutokana na mikakati mbalimbali waliyojiwekea shuleni hapo.
Tagara amewataka wazazi kuwaamini na kuwaleta watoto wao shuleni hapo ili waweze kupata elimu iliyo bora na kuweze kufikia malengo yao ya badaye huku akiwataka watoto hao kuyatunza yale yote waliyoyapata shuleni hapo na kuwa mabalozi bora wa shule hiyo.
Naye Afisa elimu kata ya Olorieni ,Digna
Swai amewataka wazazi kuwa na ushirikiano wa karibu na walimu mashuleni katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuondokana na makundi yasiyofaa.
Aidha amewataka watoto hao kujituma kwa bidii ili waweze kufikia ndoto zao huku wakijiepusha na makundi yasiyofaa badala yake waangalie kutimiza ndoto zao walizojiwekea na hatimaye kuweza kuwa mfano bora wa kuigwa kwenye jamii.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Newlife Academy ,Rogathe Kimaro amesema kuwa,wamekuwa wakijitahidi Sana kuongeza kiwango Cha ufaulu shuleni hapo kwa kuweka mikakati mbalimbali ambayo inawawezesha watoto kufanya vizuri.
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari ya Newlife Olosiva ,Piniel Laizer amesema kuwa,kwa upande wa Sekondari wamekuwa wakifanya vizuri Sana katika masomo yao ambapo kwa mwaka Jana wanafunzi 17 walipata division 1 , huku wanafunzi 14 wakipata division 2, na wanafunzi 7 wakipata division 3 hivyo amewataka wazazi kutumia fursa hiyo ya kuwasomesha watoto kwani elimu ndio hazina pekee iliyobaki .