Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Antony Mtaka, akizungumza na madiwani na watumishi wa halmashauri ya Kondoa Vijijini pamoja na kukagua miradi mbalimbali iliyopo katika halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mhe.Khamis Mkanachi,akizungumza wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Kondoa Vijijini .
Mustapha semwaiko Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Vijijini Mustapha Semwaiko akieleza namna miradi inavyoendelea katika wilaya hiyo pamoja na changamoto zake wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Kondoa Vijijini .
Mwenyekijiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa halmashauri ya kondoa vijijini,Mohamedi Kova,akichangia wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Kondoa Vijijini .
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka wakati akizungumza na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Kondoa Vijijini .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri ya Kondoa vijijini mara baada ya kuzungumza na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo.
Ujenzi ukiendelea
…………………………………………………………………….
Na Erick Mungele,Kondoa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Antony Mtaka, amewataka madiwani wa halmashauri ya kondoa vijijini kuwa umoja pamoja na kushirikiana katika maamuzi ili waweze kusimamia miradi inayofanywa katika maeneo waliopo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo RC Mtaka amesema kuwa wasipofanya na ushirikiano wataendelea kuchelewesha miradi mbalimbali.
”Kwa kweli naowaomba sana muache malumbano na majungu pamoja na migogoro yenu isiyo na tija mnasababisha baadhi ya miradi kutokamilika kwa wakati hivyo nawaomba mfanye kazi kwa ushirikiano na vitendo ili maendeleo yaweze kuwafikia wananchi’amesema Mtaka
Hata hivyo Mtaka amekagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika halmashauri hiyo pamoja na utekelezaji wa miradi hiyo ni pamoja na hospitali ya wilaya na shule kutokana na fedha za uviko 19 inayotarajia kamilika feb, 2022.
”Kwa kweli nimekagua miradi hii ila kiukweli sijaridhishwa kabisa na kasi ya miradi yote miwili hivyo natoa siku kumi ilikujitafakali na kuahidi kufanya kikao na watumishi wote wa halmashauri”
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mhe.Khamis Mkanachi, amekili kutokwepo kwa ushirikiano katika kutekeleza miradi inayotekelewa katika wilaya yake na kuahidi kuweza kusimamia na kukamilika kwa wakati.
Amesema changamoto zinazoendelea katika miradi ni kutokana na wasimamizi kutokuwa wazi na kufanya kutoendelea kwa kazi nakufanya miradi kucheleweshwa maana amekuwa akikagua mara kwa mara.
“kama ulivyojionea ndio hali ndio hali halisi ya kutokuwepo kwa ushirikiano baina yetu na watumishi wa halmashauri ila nitaweza kusimamia na kukamilika kwa wakati.
Naye Mwenyekijiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa halmashauri ya kondoa vijijini,Mohamedi Kova ,ametoa ushauri kwa mkuu wa Mkoa kuwasamehe kutokana na kucheleweshwa kwa miradi na kuwapa muda kutokana na miradi kucheleweshwa.
Aidha amepongeza mkuu wa mkoa kwa kuendelea kupambania jiji la Dodoma nakumuomba kuweza pia kupambania kondoa kurudi katika hali yake kama zamani katika kielimu , afya na kiuchumi.
“Kutokana na jitihada zako ningependa kukushukuru kwa kuendelea kupambania jiji la Dodoma pia na kondoa ili iweze kurudi kama zamani maana tulikuwa tunatamba katika vikao vya mkoa ila sasa tunakuja na sababu zisizoeleweka ni vyema utupambanie wewe, ” amesema