Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Mkutano na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi ya UVIKO 19 sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi kuwapa maelekezo namna ya kutekeleza miradi hiyo leo Oktoba 30,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Maryprisca Mahundi akizungumza na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi ya UVIKO 19 sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi kuwapa maelekezo namna ya kutekeleza miradi hiyo kilichofanyika leo Oktoba 30,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa Mkutano na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi ya UVIKO 19 sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi kuwapa maelekezo namna ya kutekeleza miradi hiyo.
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya mamoja na wakurugenzi wa mamlaka za maji mara baada ya kumalizika kwa mkutano wakati alipokutana na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi ya UVIKO 19 sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi kuwapa maelekezo namna ya kutekeleza miradi hiyo.
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya mamoja na watendaji wa Wizara ya Maji mara baada ya kumalizika kwa mkutano wakati alipokutana na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi ya UVIKO 19 sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi kuwapa maelekezo namna ya kutekeleza miradi hiyo.
Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wakati alipokutana na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi ya UVIKO 19 sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi kuwapa maelekezo namna ya kutekeleza miradi hiyo.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna, Dodoma.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewaagiza watendaji wa Wizara na wakandarasi na wasimamizi watakao simamia fedha za miradi 218 ya fedha za UVIKO 19 kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya miezi 6 hadi 7 na kwa ubora mkubwa ili wananchi waanze kupata huduma ya maji.
Waziri Aweso ameyabainisha hayo Jijini Dodoma wakati alipokutana na watendaji wa Wizara, mabonge, wakurugenzi wa mamlaka za maji mijini na vijijini watakao tekeleza miradi hiyo sambamba na wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vya ujenzi.
Waziri Aweso amesema miradi hiyo ni muhimu na lazima imalizike ndani ya miezi sita hadi saba na itekelezwe kwa ubora ukubwa na miradi hiyo iwe endelevu ili wananchi wapate huduma ya maji kama adhima ya Rais Samia katika kuwapa huduma wananchi.
“Najua Rais alitoa miezi 9 miradi hii ikamilike lakini mimi nataka miezi 9 inapofika miradi yote iwe imekamilika ninyi mkamilishe ndani ya miezi 6 hadi 7” amesema Waziri Aweso.
Ameongeza kuwa “Najua wakandarasi tunao tena wenye uwezo wa kufanya kazi nzuri tu pale Dumila kwa mda mrefu tulikosa maji lakini niliagiza wamefanya tena vizuri naamini hata hii miradi itatekelezwa kwa ubora mkubwa hivyo hivyo Handeni” amesema.
Aidha Waziri Aweso amewaonya wakuu wa idara za manunuzi kuhakikisha wanaondoa michakato mirefu isiyokuwa na ulazima katika kutekeleza miradi hiyo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Pia ameagiza kila mradi utakaokuwa unatekelezwa kuhakikisha unakuwa na jarida lake ili wakati wa ukaguzi au kiongozi yeyote atakayetaka taarifa zipatikane kwa wakati tangu mwanzo wa mradi hadi mwisho wa mradi.
Waziri Aweso amesema yeye na viongozi wengine wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanafuatilia miradi hiyo huku akionya hakuna fedha ya mradi huo kwenda kwenye kulipana posho na wale watakaotumia vibaya fedha hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Kuna wengi humu ndani hayajapitiwa na COVID 19 lakini muwe makini munaweza kupatwa na fedha za UVIKO 19 kwakweli atakayechezea fedha hizi hataachwa salama kabisa natoa onyo tena” amesema.
Pia amewataka wasambazaji na watengenezaji wa vifaa vitakavyotunika katika miradi hiyo kutekeleza kwa kuzingatia ubora ili miradi hiyo inayotekelezwa iwe katika ubora mkubwa.
Awali Naibu Waziri wa Maji Mhe. Marprisca Mahundi amesema mbali na miradi ya uviko 19 katika maeneo mengi hapa nchini kuna miradi mingine inatekelezwa nayo isimamiwe kikamilifu na ikamilike kwa wakati wananchi wapate huduma.
Pia amewataka kuzingatia nidhamu katika kazi na kila mtu amuheshimu mwenzake na kila kiongozi aheshimiwe kutokana na kofia yake na kuondoa mambo ya kujuana kwani mambo hayo yanapelekea utoaji huduma usiozingatia viwango.