………………………………………………………..
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
SERIKALI imetoa kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia tatu na tisini kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 65 vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza 2022.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema katika kikao cha Baraza la kazi kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mgema amewataka watendaji wote wanaohusika katika utekelezaji wa ujenzi wa madarasa hayo kujiepusha na ubadhirifu wa aina yoyote kwani atakaye bainika hata mfumbia macho,na wahakikishe wanashiriki kusimamia miradi hiyo kikamilifu ili thamani ya fedha itoe tija kwenye mradi husika
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo BNeema Maghembe ametoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo kuwa shilingi milioni 920 zitatumika kujenga vyumba vya madarasa 46 kwa shule za sekondari 16,na shilingi milioni 380 zitatumika kujenga madarasa katika vituo shikizi vya shule za msingi.
Maghembe amevitaja vituo shikizi vitano ambavyo vimenufaika na mgao huo kuwa ni Ligunga,Lunyeri,Jenister,vingine ni Mhimbasi na Lihuhu ambavyo vyote vimepata mgao wa shilingi milioni 20 ambazo tayari zimeingizwa kwenye akaunti za shule hizo kadiri ya miongozo ya Serikali.
Amezitaja shule za Sekondari ambazo zimenufaika na mgao huo kuwa ni Namihoro,Maposeni,Ndongosi,Namatuhi,Barabarani,Mpitimbi Lupunga,Mhalule na shule nyingine kuwa ni Matimira,Darajambili,Magagura,Nalima,Litapwasi,Muhukuru,Liganga na Kilagano fedha hizo tayari zimeingizwa katika akaunti za shule hizo.
Ameishukuru Serika kwa kutoa kiasi hicho cha fedha ambacho kinakwenda kumaliza tatizo la vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza mwaka 2022 katika maeneo hayo yaliyoainishwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumla ya shule za Sekondari 16 nashule za msingi 73 zinazomilikiwa na Serikali.