Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba akiwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan. Ujumbe huo umepokelewa na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan.
Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan akiuangalia ujumbe wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan aliokabidhiwa na Waziri Makamba kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan .
Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga
……………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu,
Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (Mb), amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan.
Mhe. Makamba amewasilisha ujumbe huo Maalum kupitia kwa Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, tarehe 24 Oktoba 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya UAE.
Waziri Makamba yupo nchini Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala Mafuta na Gesi.
Waziri Makamba ameambatana na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga, Kamishina wa Nishati na Gesi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Petroli Nchini (TPDC).