Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Rais wa Foundation for Civil Society(FCS), Dk. Stigmata Tenga,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu wa Asasi, Mussa Sang’anya,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha utawala bora kutoka Ubalozi wa Uswiz Bi.Sacha muller, ,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano kutoka ubalozi wa Denmark Mette Bech Pilgaard,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Kaimu Balozi wa Canada Bi.Helen Fytche ,akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza leo Oktoba 23, 2021 Jijini Dodoma.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Faki Shawei akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara na kupata nyaraka mbalimbali ikiwemo nakala ya sheria ya uendeshaji wa Mashirika.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wende Saga akimsikiliza mwananchi aliyetembelea Banda la Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii katika uzinduzi wa wiki ya Asasi za Kiraia leo tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma.
…………………………………………………………………..
Na Alex Sonna, Dodoma
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amezitaka Asasi za Kiraia(AZAKI) kuwa wazalendo na waadilifu kwa maslahi mapana ya nchi yao na wasikubali kutumika.
Ndugai ameyasema hayo leo Oktoba 23,2021 wakati akifungua maonesho ya Wiki ya AZAKI yanayofanyika jijini Dodoma.
Amezitaka asasi hizo kuwadhibiti watu wenye tabia zisizo vumilika na wasikubali kutumika huku akiwahakikishia kuwa uongozi wa nchi unawapenda wanaazaki kutokana na mchango walio nao kwenye maendeleo ya watanzania.
Amesema kuwa Bunge lipo tayari kama Asasi hizo zitataka kutoa elimu kwa mambo mbalimbali ambayo wangependa wabunge wapate kwa kuwa zina mchango mkubwa kwenye maendeleo ya taifa.
“Ujumbe wangu wa leo msikubali msikubali kutumika ninyi ni vijana wetu ni watanzania kama watanzania wengine, tusijenge utamaduni wa kuisemasema nchi yetu kama vile tuna nchi nyingine, ipendeni sana nchi yetu, jitoeni sana kuijenga nchi yenu, viongozi wenu hawa ni watu wema ni wazuri ni binadamu wa kawaida.”
“Nikisema mama Samia ni mtu mwema natoa rohoni, mtu mwema sana na wasaidizi wake, hata Bunge sisi ni watu wema tu, Mahakama chini ya Jaji Mkuu ni watu wema, mnafikiri hizo nchi za wengine zinaongozwa na malaika, si kweli…Hatuwezi kuwa perfect kwenye kila kitu ukitukosoa tutasikiliza lakini siku zingine jitokezeni mtupongeze pale ambapo tumefanya vizuri,”amesema.
Awali, Rais wa Foundation for Civil Society(FCS), Dk. Stigmata Tenga, amesema asasi hazishiriki kikamilifu katika mabadiliko ya sera na sheria nchini.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu wa Asasi, Mussa Sang’anya, amezitaka asasi kutokuwa na mashaka kuhusu mabadiliko ya sheria namba tatu ya mwaka 2019 inayoweka ukomo wa miaka 10 kwa vyeti vya usajili wa mashirika hayo.
Amesema lengo la serikali kuweka ukomo ni kuhuisha taarifa na kusaidia kutambua mchango wa mashirika katika kufikia maendeleo ya wananchi.
Ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha wanafuata Sheria, Kanuni na miongozo iliyowekwa na Wizara na kwamba ipo tayari kushirikiana nao kwa maslahi ya taifa.