Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Herry James akizungumza na kutoa nasaha zake katika sherehe hizo za kuhitimu vijana wapatao 109 ambao wamepatiwa ufundi stadi kutoka chuo cha VETA kwa ufadhili wa shirika la Ocode.
Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson wa kulia akizungumza jambo wakati wa halfa hiyo ya kuhitimu vijana 109.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo akiwa na viongozi wa shirika la ocode, pamoja na viongozi wa chuo cha Veta na baadhi ya wahitimi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi cheti mmoja wa vijana amabao wamefanikiwa kuhitimu mafunzo mbali mbali katika chuo cha Veta.
****************************
NA VICTOR MASANGU
VIJANA wengi katika maeneo mbali mbali hapa nchini wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa ajira hivyo baadhi yao wanapomaliza elimu ya msingi wanajikuta wanashinda vijiweni na wanashindwa kujishughulisha katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali au kuweza kujiajiri ili kuweza kuondokana na wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi.
Katika kuliona hilo Shirika la kitaifa lisolokuwa la kiserikali la Organizatioo for Community Development (OCODE) limeamua kuja na mikakati kabambe ya kuwasaidia vijana ambapo limefanikiwa kuwawezesha vijana wapatao 109 kwa kuweza kupatiwa mafunzo ya stadi za maisha pamoja na fani mbalimbali kupitia chuo cha ufundi VETA ambapo wamefanikiwa.
Shirika hilo la Ocode ambalo linafanya shughuli zake katika Manispaa ya Ubungo kwa kupitia mradi ujulikanao kwa jina la Bonga ambao umejikita zaidi kwa kuwahusiha vijana kuanzia umri wa miaka 13-19 ambao hawakuweza kupata fursa ya kuendelea na mfumo rasmi wa elimu hivyo kupitia stadi za maisha imewawezesha vijana hao kujitambua, pamoja na kutatua matatizo yao.
Akizungumza katika mahafali hayo ambayo yamewajumuisha vijana 109 kutoka maeneo ya Buza, Kipawa pamoja an Chang’ambe Mkurugenzi wa shirika hilo ndugu Joseph Jackson alisema kuwa mafunzo waliopatiwa vijana hao yatakuwa ni cahachu zaidi ya kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa upande wao pamoja na kuisaidia jamii.
“Mimi kama mkurugenzi napenda kusema kwamba haya mafunzo kwa vijana hawa itakuwa ni moja ya hatua kubwa sana kwa upande wao na italeta chemchem ya Maendeleo dhidi yao na kwamba hii ni kama mbegu kwenu hakikisheni kila mmoja anaenda kuizalisha na kubadili kabisa mfumo wake wa maisha kupitia ujuzi aliopatiwa tukumbuke kuwa mafunzo bila vitendo ni sawa na bure,”alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake mgeni rasmi wa mahafali hayo mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ndugu Herry James alibainisha kuwa wao kama serikali wanatambua mchango mkubwa ambao uanfanya na shirika la Ocode katika kuwasaidia vijana kuwawezesha kuwapeleka katika vyuo vya veta kwa lengo la kupata ujuzi mbali mbali ambao utawasaidia katika kujiajiri.
“Nipende kulipongeza shirika hilli la Ocode kwa kuweza kutoa sapoti kubwa kwa jinsi ya kuonyesha jitihada za za hali na mali kwa kuwasaidia vijana hao ambao wapo 109 na wamehitimu katiak chuo cha veta hivyo siis kama serikali tunaahidi kutoa fedha kwa vijana hao kulingana na mahitaji yao ila kwa vikundi vya watu wasiopungua watano”.alisema James.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya aliwasisitiza viongozi wa halmashauri kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele zaidi kwa vijana hao ambao kwa sasa wana nia na udhubutu mkunwa katika kujaribu kufanya vitu mbali mbali katika kubadili mfumo wa maisha yao pamoja na kuisaidia jamii kupitia fani mbali mbali na ujuzi walioupata.
Kadhalika hakusita kuwasihi wahitimu wote kuachana na tabia ya kubweteka kutokana na elimu amabo wameipata na badala yake waweke misingi imara ya kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuweza kutimiza ndoto zao waliojiwekea katika maisha ya baadae.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha VETA kipawa ndugu Sostenes Mkasanga ameshukuru kwa dhati ushirikiano uliopo baina yao na shirika la OCODE na kwamba wana imani kuwa wataendelea zaidi ufanya kazi pamoja na kwa pamoja tutaweza kufikia ndoto za vijana wengi waliokata tamaa ya kuendelea mbele kimaisha.
Doreen Matekele ni Meneja mradi wa ustawi wa jamii kutoka shirika la Ocode ambapo amesema kuwa nia malengo yao makubwa ni kuwazesha vijana hao kuwapatia stadi za maisha ili kuweza kukabiliana na chanagmoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo kuwapatia mafunzo ya ufundi kwa kushirikiana na uongozi wa Veta.
SHIRIKA hilo la Ocode katika kuwaweshesha elimu hiyo ya veta vijana wapatao 109 limeweza kutumia kiasi cha shilingi shilingi milioni 102 kwa vijana hao ambao wamehitimu fani mbali mbali ikiwemo ya udereva, mapambo,ufundi magari, saloon, ufundi simu ,mapishi na ufundi umeme.