Mkurugenzi wa Tehama wa wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari ,ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mkutano wa Tano wa mwaka wa Tehama,Mulembwa Munaku akizungumza na waandishi jijini Arusha.(Happy Lazaro).
***************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgenirasmi katika kufunga mkutano wa wadau wa Tehama unaofanyika mjini hapa .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tehama wa wizara ya habari
,Mawasiliano na teknolojia ya habari ,ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mkutano wa tano wa mwaka wa Tehama ,Mulembwa Munaku wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Munaku amesema kuwa,lengo la mkutano huo ni kukutana na wadau wa posta katika kuangalia changamoto zinazowakabili na kuweza kuziboresha na kuweza kuangalia ubobezi uliopo sambamba na kuangalia wamepiga hatua kiasi gani katika.maswala ya posta.
Amesema kuwa,wadau hao wa matumizi ya Tehama kutoka nchi mbalimbali wameweza kukutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili mustakabali wa matumizi ya Tehama huku changamoto kubwa ikionyesha matumizi ya Tehama kukua kwa kiasi kikubwa huku vijana wakiwa ndiyo watumiaji wakubwa wa mitandao hiyo.
Munaku amesema kuwa, jamii ina wajibu wa kuhakikisha vijana wanatumia Tehama kwa matumizi sahihi na sio kupotosha umma kwani endapo mitandao hiyo itatumiwa vizuri itatahusisha Sana vijana kuweza kuelimika na hata kuweza kujiajiri kupitia Tehama.
Ameongeza kuwa, hapa nchini asilimia 75 ya vijana wanatumia matumizi ya Tehama kwa namna mbalimbali ikiwemo kudhihaki baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea kadhia kwenye familia ,hivyo amewataka vijana kutumia Tehama katika kubuni vitu mbalimbali vitakavyo wapatia ajira.
“Naomba niwaombe wazazi pamoja na walezi kuwa , wana wajibu na jukumu kubwa la kuhakikisha tunawajengea misingi uliyo bora vijana wetu na kuhakikisha wanakuwa na matumizi sahihi ya Tehama katika kujiletea maendeleo.”amesema .
Amefafanua zaidi kuwa ,wizara ya habari inajikita zaidi katika kutoa elimu kwa vijana na jamii kutumia Tehama kama fursa na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.
Amesema kuwa, lengo kubwa ni kuhakikisha wanajenga Taifa la kidigitali huku wakiendelea kutoa elimu kwa vijana katika kutambua matumizi sahihi ya Tehama kwani vijana wengi hawatumii kwa ukamilifu mitandao hiyo Jambo ambalo limekuwa likileta athari kubwa katika jamii.