Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (aliyevaa suti ya kaki) akizungumza na viongozi na watumishi wa halamshauri ya wikaya ya Nkasi wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kasu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akitazama tofali zitakazotumika kwenye ujenzi wa kituo cha afya Kasu ambapo amebaini na kuagiza wahandishi kufanya uchunguzi wa ubora wa tofali 19,500 zilizofyatulia kabla ujenzi haujaanza.
……………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amesema hajaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Kasu wilayani Nkasi ambapo amebaini taratibu na miongozo kutosimamiwa kufuatia serikali kutoa shilingi milioni 500.
Ametoa kauli hiyo leo wakati alipoanza ziara ya kazi kukagua miradi ya maendeleo na kuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo William Mwakalambile kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za serikali.
Akiwa kwenye eneo la mradi Mkuu huyo wa Mkoa alibaini matumizi yasiyo sahihi ya shilingi Milioni 60 zilizotumika kati ya shilingi Milioni 500 kujenga jengo la wagonjwa wa nje kinyume na utaratibu wa fedha zilizotolewa na serikali.
“Sijafurahishwa na mwenendo wa kazi ya ujenzi hapa. Inaonekana hapa halmashauri hamjajipanga kukamilisha mradi huu unaosubiriwa mno na wananchi” alisema Mkirikiti
Serikali imetoa shilingi Milioni 500 kwa halmashauri ya wilaya ya Nkasi kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha Afya Kata ya Kasu ambapo tayari kimeanza kwa halamshauri kukusanya vifaa vya kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa wikaya ya Nkasi Peter Lijuakali amesema ataendelea kuhakikisha watendaji wa halmashauri wanazingatia matumizi sahihi ya fedha za umma huku miradi ikiwa bora.
“Nilifika hapa awali na kubaini matumizi ya shilingi milioni 60 kinyume cha utaratibu kwani jengo hilo wanalodai ni OPD likianzishwa na wananchi tofauti na fedha za serikali mikioni 500 za sasa hivyo nikaaagiza lisimame ” alisema Lijuakali.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameanza ziara ya siku mbili kwenye wilaya ya Nkasi ambapo anakagua miradi ya elimu,afya,bandari ya Kabwe na ataongea na wananchi kutoa elimunjuu ya kujikinga na maabukizo ya UVIKO-19 kwa kujitokeza kuchanja.