Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Hospitali ya Jiji la Arusha katika Eneo la Njiro Arumeru Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba 2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimsalimia mtoto Samia Yona aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jiji la Arusha muda mfupi baada ya kuziindua rasmi Hospitali hiyo iliopo katika eneo la Chekereni Arumeru Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba 2021, aliye mshikilia mtoto huyo ni Mama Mzazi Mary Joseph (34) mkazi wa Njiro Arusha. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimsalimia mtoto Nassir Mbarouk aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jiji la Arusha muda mfupi baada ya kuziindua rasmi Hospitali hiyo iliopo katika eneo la Chekereni Arumeru Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba 2021, aliye mshikilia mtoto huyo ni Mama Mzazi Shadya Samson (32) mkazi wa Uswahilini Arusha. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Chekereni Arumeru Mkoani Arusha mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa Maji safi na Salama unaoendelea katika eneo hilo leo tarehe 17 Oktoba 2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi ya shilingi milioni 387,380,675.00 kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu katika Tarafa ya Themi Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba 2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.