**********************
Na.WAMJW- DSM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambapo wamekubaliana kuimarisha mahusiano na mashirikiano kati ya Tanzania na Uswisi.
Dkt. Gwajima amemhakikishia Balozi huyo kuendelea kusaidiana na Serikali ya Uswisi na katika mazungumzo yao wote wawili wamekubaliana kufadhili uimarishaji mfuko wa afya ya pamoja (HBF), mifumo ya afya pamoja na huduma zote za mtandao katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Naye, Balozi Mhe. Didier Chassot amesema Uswisi iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya hususani katika swala zima la kuimarisha mifumo ya vituo vya afya na huduma za mtandao.
Viongozi hao wamekutaka na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Wizara mkoani Dar es Salaam, ambapo kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe OR- TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.