Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya Onesho la Kwanza la Utalii katika nchi za Afrika Mashariki (FIRST EAS TOURISM EXPO 2021) ambalo Tanzania Mwenyeji wa Onesho hilo ambalo uzinduzi utafanyika Mjini Arusha oktoba 9, 20221.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro (kulia) akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya Onesho la Kwanza la Utalii katika nchi za Afrika Mashariki (FIRST EAS TOURISM EXPO 2021) ambalo Tanzania Mwenyeji wa Onesho hilo ambalo uzinduzi utafanyika Mjini Arusha oktoba 9, 20221.
(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)
***********************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Tanzania ni mwenyeji wa Onesho la Kwanza la Utalii katika nchi za Afrika Mashariki (FIRST EAS TOURISM EXPO 2021) ambayo itafanyika kati ya tarehe 9 mpaka tarehe 16 Oktoba 2021 ambapo kutakuwa na uzinduzi rasmi Oktoba 9 2021 katika Viwanja vya TGT Mjini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro amesema kuanzia tarehe 12 mpaka 16 kutakuwa na safari za kiutalii ambapo waandishi wa habari na wananchi wote kwa ujumla ambao wangependa kwenda kwenye safari hizo za Utalii.
“Katika kuunga mkono juhudi za kutangaza Utalii wa Tanzania na kuunga mkono Royal Tour ambayo Mheshimiwa Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassani aliiyanzisha, Wizara imefuta TAX Fees kwa muda wa wiki moja wakati wa Tour”. Amesema Waziri Dkt.Ndumbaro.
Amesema tozo za Serikali kwa muda wa siku saba zote wanazisimamisha ili FIRST EAS TOURISM EXPO 2021 ipewe heshima ambayo inastahiri, wenzetu wa Afrika Mashariki wametupa heshima Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuandaa Onesho hilo na baada ya hapo kila mwaka itakuwa inaenda kwenye nchi nyingine, tukianza na Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, South Sudani na baadae itarudi tena Tanzania.
Aidha Waziri Dkt.Ndumbaro amesema kupitia onesho hilo manufaa yake ni makubwa ambapo tunatangaza vivutio mbalimbali vya utalii pia wanunuzi na wauzaji wa huduma za kitalii wanakutana wandani na wa nje ya nchi kwasababu mpaka sasa nchi zote za Afrika Mashariki zimethibiisha kushiriki na kila nchi inakuja na Mawaziri wake na Sekta binafsi katika huduma ya utalii.
Pamoja na hayo amesema African Tourism Board imethibisha kushiriki na imependa kutumia tukio hilo kutoa tuzo kwa viongozi mbalimbali ambao wamefanya vizuri katika sekta ya Utalii barani Afrika.
Amesema wanategemea mgeni rasmi atakuwa mmoja wa viongozi wa juu hapa nchini aweze kufungua na kufunga tukio hilo.Pia baadhi ya viiongozi mbalimbali barani Afrika wamethibitisha kushiriki tukio hilo.