Afisa Muuguzi, Situ Muhunzi akipokea maswali ya wananchi wa Mtaa wa Kawawa kwenye Mkutano wa hadhara
………………………………………………..
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WAKINA mama wa Kata ya Mbalawala wameshauriwa kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma za Afya pindi wanapojihisi kuwa wajawazito mapema chini ya miezi minne ili waweze kupata huduma za Afya mapema.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Muuguzi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Situ Muhunzi alipokuwa akijibu maswali ya wananchi wa Mtaa wa Kawawa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mtaani hapo.
Muhunzi alisema kuwa eneo la Lugala na Mtaa wa Kawawa wakina mama wanachelewa sana kwenda kliniki. “Kina mama wengi wanahudhuria kliniki baada ya miezi mitano. Kina mama tunatakiwa kwenda mapema kliniki ili kujua kama una tatizo tulifanyie kazi mapema. Hii itasaidia kuepukana na kujifungua watoto waliofariki” alisema Muhunzi.
Akiongelea usalama wa chanjo hiyo, Afisa Muuguzi huyo, alisema kuwa chanjo hiyo ni salama na haisababishi madhara yoyote. “Chanjo hii ni salama, na haizuii uzazi. Chanjo tumezikuta nyingi na tunaendelea kuchanja na bado tunaendelea kuzaa. Chanjo hii ni salama kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha” alisema Muhunzi.