Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Rulalo katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Rulalo juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiangalia zizi la mbuzi la mmoja wa Walengwa wa TASAF, Bi. Beatha Katushabe wa kijiji cha Rulalo wilayani Karagwe mkoani Kagera ambaye anamiliki mbuzi 25 aliowapata kutokana na ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akipokea zawadi ya mkungu wa ndizi kutoka kwa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Rukole, Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Rukole, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Bi. Rhoda Ernest (wa tatu kushoto kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akionyesha kisima cha kuvuna maji ya mvua alichokijenga kwa kutumia na ruzuku ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi ya mkeka uliosukwa na mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi.Rhoda Ernest katika kijiji cha Rukole, wilayani Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
************
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Karagwe
Mkoani Kagera, wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuwapunguzia kero ya umaskini kupitia Mpango huo unaotekelezwa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika vijiji vya Rulalo na Rukole,
wanufaika hao wamesema Mpango huo umewawezesha kuboresha
maisha yao kwa kiwango kikubwa sana.
Wamesema mkakati wa Serikali wa kupambana na umaskini kupitia
TASAF umeamsha ari ya kujiletea maendeleo na kuwawezesha kutunza
kaya zao kwa uhakika tofauti na ilivyokuwa kabla ya uwepo wa Mpango
huo.
“Hivi sasa na sisi tunaonekana watu, kwani tunaweza kujikimu na kupanga
namna ya kuendesha maisha yetu kwa uhakika, tunamshukuru sana Rais
Magufuli kwa kutujali’’. Amesema mmoja wa Walengwa katika kijiji cha
Rukole, Bi. Rhoida Ernest.
Dkt. Mwanjelwa amesema kinachofanywa na Serikali kupitia TASAF ni
sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mwenyezi Mungu ambayo hata katika Vitabu Vitakatifu vinazungumzia suala la kuwajali wasiojiweza ikiwa ni pamoja na yatima, wajane na maskini huku akinukuu Kitabu cha Yakobo: 1:27.
Dkt Mwanjelwa ameshuhudia namna Walengwa wa TASAF walivyoanzisha
miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato ikiwemo ufugaji wa mbuzi, kuku,
ujenzi wa visima vya kuvuna maji ya mvua na uboreshaji wa makazi kwa
kujenga nyumba na kuwa na uwezo wa kusomesha watoto ambao
mahudhurio yamekuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya
kuingizwa kwenye Mpango.
Amewasisitizia wanufaika hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili
kuondokana na umaskini.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa amewaagiza watendaji wa Serikali
kuwa karibu na walengwa wa TASAF ili kubaini changamoto zinazowakabili
na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati, lengo likiwa ni kuwawezesha
kujiongezea kipato na kutekeleza shughuli zao za kiuchumi kwa tija zaidi.
Ameongeza kuwa, matokeo chanya yaliyoanza kuonekana kwa Walengwa
wa TASAF yanapaswa kupewa msukumo na wataalamu hususani wa
sekta za kilimo, ufugaji na uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ambayo
itaboresha maisha yao.
Dkt. Mwanjelwa atahitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwa
kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi ambako atakutana na
wananchi na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.