***************************
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,imetimiza ahadi zake zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka Vifaa tiba Hospitali ya Wilaya ya Chalinze vyenye thamani ya Shilingi Milioni 480 .
Vifaa hivyo Ni pamoja na mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete aliishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi hii ndani ya muda wa wiki tatu toka kutolewa kwa ahadi.
Wananchi wa Kata hiyo wakiongozwa na wakina mama ambao walishukuru kwa vifaa hivyo vvitakavyosaidia kuboresha huduma ya afya na kusema Mungu amlinde Rais wa Nchi yetu.