WENYEJI Juventus jana wameutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Allianz Jijini Torino baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Kundi H bao pekee la Federico Chiesa dakika ya 46.
Ushindi huo unawapandisha kileleni Juve wakifikisha pointi sita, wakati Chelsea inabaki na pointi zake tatu sawa na Zenit, huku Malmö ambayo haina pointi ikiwa inashika mkia.