Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa bao 1-0 Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba,Mjini Bukoba Mkoani Kagera.
Shujaa wa Yanga alikuwa Kiungo Mshambuliaji Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 24 akifunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia mpira uliookolewa na kipa Issa Chalamanda kufuatia shuti la awali la mshambuliaji Mkongo, Fiston Mayele Kalala.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabao ya mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya tatu na 20 yameipa Polisi Tanzania ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha.