********************************
KAMPUNI ya SportPesa Limited ambayo inajihusisha na michezo ya ubashiri wa michezo mbalimbali, imesaini mkataba wa matangazo ya muda mrefu na kampuni ya matangazo ya Mdundo ya nchini Tanzania yenye wafuatiliaji zaidi ya milioni 9.7. Kwa kuanzia makampuni hayo yamesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Ndani ya mkataba huo wenye thamani ya dola za Marekani 100,000, kampuni ya SportPesa itawasilisha matangazo yake zaidi ya 600 ya sauti ambapo yanatarajiwa kuwafikia zaidi ya watumiaji wa Milioni 9.7 wa kampuni ya Mdundo.
Katika makubaliano hayo kampuni ya SportPesa pia itanufaika kwa matangazo yake kuwafikia walengwa wengi zaidi kutokana na umaarufu wa kampuni ya Mdundo unaotokana na bidhaa zake katika nyanja za matangazo ambazo zimekuwa na umaarufu mkubwa.
Mkataba huu ni ushahidi dhahiri ya ubunifu mkubwa unaofanywa na kampuni ya Mdundo wenye malengo ya kuwafikia na kuwaridhisha wateja wake haswa ikitiliwa maanani ya kuwa pia imeingia mikataba na makampuni mengine na yenye mafanikio makubwa yakiwemo Standard Chartered, Nivea, 9mobile, Safaricom, Coca-Cola, Guinness, Airtel, Vodacom, Carrefour Supermarket na Diageo.
Hivi karibuni kampuni ya Mdundo pia iliingia mkataba wa matangazo kupitia midundo ya muziki na makampuni ya Airtel Nigeria, MTN Nigeria na Vodacom Tanzania, ambapo kampuni hiyo ua Mdundo imechangia kwa kiasi kikubwa kwa makampuni hayo kuwafikia walengwa wengi kupitia ubunifu wake.
Mkuu wa kitengo cha chapa za bidhaa wa kampuni ya Mdundo, Rachel Karanu, anasema “Kujenga mazingira mazuri ya thamani ya kibiashara ya bidhaa za wateja wetu ndiyo msingi muhimu wa kampuni yetu na ambayo yatakuwa endelevu. SportPesa ni taasisi yenye wabunifu na wenye mawazo yenye umakini mkubwa kwa malengo ya kupata matokeo chanya; matarajio yetu ni kufanya kazi na timu yenye malengo ya matokeo chanya iliyoko Sportpesa”.
SportPesa Limited imeanzisha chapa ya kibiashara inayoongoza nchini Tanzania kutokana na umakini mkubwa unaotokana na matumizi ya uhakika wa data katika kuboresha bidhaa zake, mkakati ambao unaakisi bidhaa iliyoanzishwa mapema mwaka huu na kampuni ya Mdundo yenye lengo la kukuza chapa za bidhaa ambazo zitachangia kuboresha mapato yanayotokana na uwekezaji kupitia matangazo ya biashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SportPesa Tarimba Abbas anasema “Tumefurahi sana kwa kuanza kufanya kazi na kampuni ya Mdundo kupitia mradi huu mradi huu, hasa ikitiliwa maanani mafaniko ambayo taasisi zingine zimeshapata kupitia ubinifu wa kampuni ya Mdundo”.
Amesema kuwa tangu ilipoingia mkataba wa matangazo na kampuni ya Mdundo bidhaa za Sportpesa zimekuwa na ongezeko la aslimia 48 miongoni wa wateja wake huku kukiwa pia na maboresho kwenye nyanja zote nne za ufahamu, uzingatiaji, kupendwa zaidi na dhamira njema katika manunuzi ya bidhaa za Sportpesa.
Huduma hii inayoongoza kwa matangazo kupitia mtiririko wa muziki umezindua toleo jipya kupitia mpango wake wa kukuza bidhaa ujulikanao kama brand lift tool, wenye lengo la kutangaza chapa za makampuni ambayo ni wateja wake, kwa malengo ya kufikia masoko yaliyokusudiwa.
Mpango huo wa kukuza chapa za bidhaa utaendelea kupatikana bure kupitia mtandao wake wa Mdundoforbrands ambapo utatoa huduma kupitia data zake matangazo ya aina zaidi 30 ya bidhaa zikiwemo vyakula, Vinywaji, mawasiliano, huduma za Kifedha, huduma binafsi za matunzo pamoja na huduma za mapambo majumbani.