Makamu Mwenyekiti wa bodi ya benki ya biashara ya DCB ,Zawadia Nanyaro akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya ukaguzi wa ndani unaofanyika jijini Arusha.
Mjumbe wa bodi ya IIA ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Africanmark services, Berthasia Ladislaus akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya ukaguzi wa ndani.(Happy Lazaro).
………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Aliyekuwa Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali CAG ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa Taasisi  ya  Wajibu ,Ludovic  Utoh amesema kuwa,kuna umuhimu mkubwa Sana wa kuwepo kwa swala la uwajibikaji katika taasisi na makampuni mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi yetu.
Ameyasema hayo  wakati akizungumza katika mkutano wa  nane wa wakuu wa Taasisi za serikali na binafsi  wenye mada kuu ya uwajibikaji katika kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla ulioandaliwa na  Taasisi ya ukaguzi wa ndani unaofanyika mjini hapa.
Amesema kuwa,kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwepo kwa uwajibikaji katika sehemu mbalimbali ili ziweze kuleta maendeleo katika maeneo husika.
“Nawashukuru Sana Taasisi hii ya wakaguzi wa ndani kwa kuandaa mkutano huu ambao unalenga  kukumbushana na kuelimishana katika kuangalia uwajibikaji na nafasi ya wakaguzi wa ndani katika kuleta maendeleo yetu na ya nchi kwa ujumla kwani kila mmoja wetu anatambua kuwa  hakuna maendeleo yanayoweza kuja bila uwajibikaji  mahali popote.”amesema .

Utoh amesema kuwa,kupitia mkutano huo wanaangalia umuhimu wa uwajibikaji na maendeleo katika nafasi ya taaluma ya ukaguzi ili kujua wao wanahusikaje  kwa sababu nchi inalilia sana maendeleo na watanzania wanahitaji Sana maendeleo .
Amefafanua zaidi kuwa,watu wengi Sasa hivi wanaona umuhimu wa wakaguzi wa ndani kwani wapo kuwashauri na kuwalekeza wasimamizi  na wakuu wa mashirika na Taasisi katika kufanya vizuri kwenye utendaji kazi wao.
Mmoja kati ya  waandaji wa tamasha hilo,Zelia Njeza  amesema kuwa,lengo  la tamasha hilo ni kutoa elimu kwa wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ambapo kwa mwaka huu wanalenga kutoa elimu juu ya  uwajibikaji na utawala bora katika maendeleo ya Taasisi na Taifa kwa ujumla.
“lengo la kutoa elimu hii ni kuhakikisha wakurugenzi wa bodi mbalimbali  Tanzania  tunawawezesha kutoa huduma vizuri ,huku dhana kuu ya uwajibikaji kwa maendeleo mapana ya taasisi na nchi  kwa ujumla.”amesema Njeza.
Amefafanua kuwa,wamefikia hatua ya kutoa mafunzo  hayo  kwa lengo la kukumbushana utendaji kazi wao kwani ili uweze kuwa kiongozi mzuri lazima uendelee  kujifunza kila siku kulingana na mabadiliko ya teknolojia   na hatimaye kuweza kuwa wakuu wanaotambulika sio Tanzania tu hata duniani kwa ujumla.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya biashara ya DCB ,Zawadia Nanyaro  amesema kuwa,mkutano huo unajumuisha wajumbe wa bodi na wanaosimamia kamati.za ukaguzi ambapo alisema ni mkutano muhimu Sana kwa  wakurugenzi wa bodi mbalimbali kwani wanaweza   kupata taarifa na mafunzo namna ya kusimamia kampuni zao .
Amesema kuwa,bodi ya uongozi ndo ina mamlaka  hivyo kupitia mafunzo hayo viongozi hao wanapata fursa ya  kujifunza  na kuongea katika vikao vyao. 
Naye Mjumbe wa bodi  ya  IIA ,Berthasia Ladislaus amesema kuwa,lengo  ni kutoa elimu endelevu katika ukaguzi kwenye utawala bora na uwajibikaji  kwa wadau kutoka Serikali na Taasisi binafsi  .
Amesema kuwa,wanakutana kubadilishana mawazo katika uwajibikaji  na maendeleo kwani  wakaguzi wa ndani wana mchango mkubwa Sana katika maendeleo ya nchi na Taasisi hivyo  ili kuwasaidia lazima kuwepo na mafunzo kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao   na hatimaye  Taasisi zao ziweze kuwa salama zaidi.
Amefafanua kuwa,wanapozungumzia swala zima la maendeleo lazima watu wafahamu na wasimamie katika kuona rasilimali zinatumika upasavyo  ili kufikia malengo  yaliyowekwa kwani bila kuwepo kwa wakaguzi wa ndani huenda rasilimali zisitumike ipasavyo.