………………………………………………………………………..
VIKUNDI 23 vya ujasiriamali Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wamepatiwa kiasi cha milioni 100 kutoka asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni vikundi vya akina Mama, Vijana na watu wenye Ulemavu kama ilivyo lengo la Serikali.
Akiongea wakati wakutoa mkopo huo kwa wanavikundi hao Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo amewatahadharisha wanavikundi hao kutumia pesa hizo katika kusudi walilojiwekea ilikufikia malengo ya kikundi ikiwa ni pamoja na kurejesha mkopo huo kwa wakati.
Mpogolo amesema vipo baadhi ya vikundi ambavyo sio vimekosa uaminifu na kupewa mkopo na Serikali kwalengo la kuwajengea uwezo lakini ulipaji umekuwa wa kusuasua na kuvikosesha vikundi vingine kupata mkopo kwa wakati.
“Tuna wapa mkopo leo nendeni mkafanye shughuli mliyoombea mkopo huu na sivinginevyo ili kuweza kufikia malengo na kuweza kurejesha kwa wakati”
“Amesema Mpogolo”
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo ya Same Annastazia Tutuba akitoa taarifa ya utoaji wa mkopo huo amesema katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021-2022 kupitia mapato ya ndani wamefanikiwa kutenga kiasi hicho cha milioni 100 kwaajili ya kuyawezesha makundi hayo ilikuweza kujikwamua.
Tutuba amesema Serikali Imekuwa ikitoa maelekezo kila siku kuhusu halmashauri kutenga fedha kwaajili ya makundi hayo hivyo wao kufanya hivyo nikutekeleza maagizo ya Serikali.
“Tumekuwa tukielekezawa na Serikali kuu kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya makundi haya hivyo leo tumewapatia vikundi 23 milioni 100 ikiwa ni akina Mama, Vijana na watu wenye Ulemavu kama mlengwa wa Serikali utavyotutaka”
“Amesema Tutuba”
Amina Hassani ni mmoja wa wanavikundi toka kundi la akina Mama ambao wamepatiwa mkopo amewataka wanavikundi wenzake kuhakikisha wanatumia fedha hizo katika shughuli za kujiletea maendeleo na kurejesha mkopo kwa wakati.
Mercy Shandala ni mratibu wa vikundi toka idara ya maendeleo ya jamii Wilayani Same amewataka wanavikundi hao kujiwekeza zaidi Katika nyanja ya viwanda kama walivyoomba ilikunugaisha jamii na shughuli ziweze kujitangaza Katika maeneo mbalimbali ndani na hata nje ya Taifa.